Njia 6 Za Kuuteka Nyara Moyo Wa Mwanamke
Je ungependa kujua na kufahamu mbinu za kumteka nyara mwanamke na kumfanya awe wako milele?
Relax, zama nami huku nikikueleza hatua za moja kwa moja za kufuata.
Kuteka nyara moyo wa mwanamke
1. Jizuie kumwambia hisia zako mapema
Ingawaje ni vizuri kumsifia mwanamke mara kwa mara, kumwambia hisia zako
kwake ni jambo ambalo nalipinga. Unafaa umpatie muda wa kumfanya
azungukwe na mawazo na maswali kukuhusu. Pia ni vizuri ujenge tenshen ya
mapenzi kati yenu. Kando na haya yote, hisia zako kwake zinaweza
kupotea baada ya miezi mifupi kama iwapo utagundua ya kuwa hamgawi
maslahi yanayowiana.
Hivyo, kama unampenda mwanamke jipatie muda mrefu wa kumsoma kabla
hujamwambia chochote. Labda unaweza kumkeep buzy kwa kuingia kwa akili
yake.
2. Mpe atenshen kwa kuwa makini
Ok najua unamuuliza maswali yafaayo ambayo yanamfanya avutiwe nawe,
lakini swali ni je unamakinika na yeye ama ni runinga ama ni simu yako
ndio inakukeep buzy?
Kosa ambalo wanaume wengi hufanya ni kutomakinika wakati ambapo wanazungumza na mwanamke.
Kama kweli umepatikana na dharura basi ni bora kumwomba ruhusa ya
kupokea simu nk. Kama hauna dharura yeyote, basi ni vyema kwako
kumakinika na yeye. Bila hivyo mwanamke kama huyo ataona kama
unampotezea wakati.
3. Jitenge na vifaa vya elektroniki
Baada ya kugusia swala la kumpa atenshen hapo juu, unafaa kujitenga na
simu zako zote wakati ambapo unamtoa mwanamke deti ama out. Kama
utashindwa kujizuia basi weka simu yako silent ama uizime kabisa ili
usiingiwe na mawazo ya kufikiria simu yako.
Kufanya hivi hakutakupa nafasi ya kumakinika kwa mwanamke pekee, bali
pia kutakusaidia wewe kuwa mbunifu, kuwa bila stress za kusumbuliwa
kutaka kupokea simu za huyu na yule. Akili yako inatulia na kumakinika
kwa kitu kimoja. Mwanamke.
Mwonyeshe ya kuwa unadhamini kikao chake na wewe. Mwonyeshe ya kuwa yeye ndiye kila kitu wakati huo na hauko tayari kupoteza muda huo ulionao na yeye kwa maswala mengine.
Mwonyeshe ya kuwa unadhamini kikao chake na wewe. Mwonyeshe ya kuwa yeye ndiye kila kitu wakati huo na hauko tayari kupoteza muda huo ulionao na yeye kwa maswala mengine.
Kumbuka: Njia ya kuuteka nyara moyo wa mwanamke ni kuwa na maongezi ambayo yatamfurahisha na kumpendeza.
4. Hakikisha kila kumvutia kunahisabika
Kila mwanaume anafahamu umuhimu wa kumvutia mwanamke, lakini si kila
mwanaume anafahamu umuhimu wa kila hatua ya kumvutia mwanamke. Wakati
ambapo utakuwa unaongea na mwanamke, hakikisha ya kuwa kila kitu
unachofanya unakichunguza na kutathmini. Hii nikuanzia miondoko yako ya
mwili hadi hadi mwonekano wako.
Mwonyeshe wakati wote kuwa unajiamini na bila kusahau ya kuwa unajali
maisha yako na ya wengine. Ukitelekeza chochote ambacho awali umemwambia
basi kunaweza kuwa na tatizo kati yenu.
5. Msifie
Hapa ndipo wanaume wanapenda sana. Kumsifu mwanamke.
Well, hapa mnyeshee kwa kumsifu mara kwa mara lakini usipitishe mpaka.
Iwapo kama umekuwa unadeti mwanamke kwa miezi sasa ni vyema zaidi
kumsifia mara kwa mara ili usimfanye aone ya kuwa umechoshwa na
mahusiano yenu.
Kutomsifu mwanamke kwa muda mrefu kunatoa nafasi kwa wanaume wengine kuona mwanya wa kutumia kukuangamiza.
6. Usifiche siri yeyote
Kama unataka kuuteka nyara moyo wa mwanamke, basi usijaribu kumficha
jambo lako lolote lile. Ufungue moyo wako na umwelezee chochote kile
ambacho unaona anafaa kujua. Hii ni kuanzia changamoto unazopitia,
maisha yako ya usoni na mambo mengine yanayofanana. Kufanya hivi
kutamfanya mwanamke huyu kuona ya kuwa unamjali yeye. Wanawake hupenda
wanaume ambao hawayafichi mambo yao. Well, si lazima umueleze kila kitu
hapa. Muhimu ni kuwa unamwelezea mambo muhimu ambayo unayaona ya kuwa
yanaweza kumuathiri kwa njia moja au nyingine.
Ulikuwa ukiyajua haya yote? Kama ulikuwa huyajui mpira uko kwako sasa.

Leave a Comment