BARUA YA WAZI KWAKO! Tafadhali isome utajifunza kitu

Najua hautamani kusikia lolote kutoka kwangu kwa kuwa sina thamani tena kwako, thamani niliyokuwanayo kabla hujanipatia ujauzito mara mbili zote ukanisihi nitoe. Kwa sababu ninakupenda nilifanya yote unayotaka.
Ulipodai kuwa ukitumia kinga hujisikii raha sikuogopa kuibeba mimba ya tatu. Hakika nilijitoa kwakobkwa kuwa nilikuwa mwehu wa penzi lako.
Nilifanya haya nikiamini kuwa nalinda penzi langu kwako!!! Naumia sana leo unaponiita mimi Malaya!!! Mjinga tena mshamba!! Hakika hujakosea maana nilikuwa Malaya katika chumba chako, chumba ulichonifanya utakavyo tena kila siku, huku jukumu la kukisafisha ukiniachia mimi, kweli nilikuwa mjinga sana kwa kukulilia hata pale ulipokuwa umenikosea waziwazi.
Baba si unajua nilianza uhusiano na wewe maziwa yangu yakiwa wima, mbona leo wanifukuza ukidai kuwa hunitaki kwa kuwa nina maziwa makubwa tena yamelala. Hukumbuki ni wewe uliyeyafanya hivi???
Unaniita mimi mchafu sasa unasahau kuwa ni wewe u mchafu zaidi yangu, au unasahau jinsi ulivyokuwa mchafu kupitiliza, uchafu wako uolitokana tamaa zako za kimwili tamaa zilizokufanya ulitake penzi langu hata nilipokuwa katika siku zangu!!!!! Hukuwa ukiuona uchafu huu ati leo waniita mchafu!!!
Wewe una usafi gani???
Babaa!!! Nakuandikia haya japo utayapuuzia lakini unaujua ukweli kuwa nilikupenda na wala sio kimakosa. Nilifanya yote uliyoyataka lakini hunilipi thamani yangu tena leo hii.
Unazuga kuwa u wa mjini sana!!! Unasahau kuwa ulikuwa unakosa hata pesa ya nauli nikawa nakupatia akiba yangu ya pesa nilizonazo.
Niliacha kulipa ada yangu nikakupatia pesa umnunulie mama yako dawa alipokuwa anaumwa, sijali sana hata kama ulinidanganya lakini nilifanya kwa mapenzi yangu kutoka moyoni.
Hivyo visichana vimekudanganyishia hayo mavazi yao kama viko uchi vile, macho yao ya wiziwizi yamekukamata unanisahau unasema ulipitiwa yaani ulinipenda bahati mbaya.
Ulinipenda bahati mbaya????
Wakati ulikuwa unanililia, huku ukinipigia misele kila siku nyumbani kwetu utafikiri gari ya mashindano! Hivi kumbe machozi yako yalikuwa ya kunilaghai nashukuru umefanikiwa.
Lakini naomba nikwambie kitu kimoja babaangu, ulipoamua kujiingiza katika uhusiano na visichana vyako hivyo nilivumilia lakini siku nilipokufumaniana yule rafiki yangu Jane mkifanya ngono chumbani kwako niliumia sana.
Na ni siku hiyohiyo niliamua kujibu maombi ya yule rafiki yako Benard ambae alikuwa akinitongoza kila siku, siku hiyo nililala kwake, nilizini naye kwa hiari kwa lengo la kulipiza kisasi.
Kisasi kile hakikuyatuliza maumivu yangu, bado ulikuwa una nafasi katika moyo wangu!!!
Penzi lako halikuwa na mrithi baada ya miezi kadhaa nilipata hamu ya kuwa na wewe nikaja kwako. Tukafanya mapenzi bila hata kukukumbushia juu ya uchafu ulionifanyia.
Nadhani lilikuwa kosa kubwa, kama ninavyokuandikia wewe barua hii usiyoipenda na mimi Benard aliniandikia. Na yeye aliandikiwa na Jane akadhani ni utani kumbe ni kweli tupu. Jane amethirika, amemwambukizwa na Bernard, Bernad kaniambukiza mimi halafu MIMI na JANE tumekuambukiza wewe.
Na mpaka hivi sasa hapa nilipo ninaugulia gonjwa la gono, bila shaka na wewe unalo!
Sikupenda iwe hivyo lakini na wewe sikulaumu!!!
Asante kwa kuisoma barua yangu, sina uhakika na maamuzi utakayochukua.
**************
JIULIZE MPO WANGAPI?
Leave a Comment