Barua kwa Mwanangu ambaye hajazaliwa bado



Funzo kwa wote.
Binti yangu mpendwa,
Nimekuwa nikikufikiria sana hivi karibuni, na jioni hii hakuna kingine ninachokihitaji zaidi ya kuongea na wewe.
Lakini kwa kuwa haupo hapa muda huu nimeamua kuucha huu ujumbe uje kuusoma pale utakapokua mkubwa, nisije huko mbeleni nikasahau ni nini nilikuwa nikitaka kuongea na wewe.
Ni hivi,
Maisha yako ni ya thamani mno kwangu mwanangu, hivyo siwezi kuiacha nafasi yoyote napopata wasaa wa kuzungumza yaliyo mema kwako. Najua utaisoma hii siku moja.
Kuna nyakati mbaya kabisa katika maisha, zitategemeana sana ni jinsi wewe ulivyoyachukulia maisha. Kuwa na amani na kila mtu, ila usihangaike kumuabudu mtu hata siku moja.
Haitajalisha ni kiasi gani umejaribu, lazima utafeli tu kumuabudu kila mtu, jinsi utakavyozidi kumuabudu huyu, ndivyo utakavyozidi kumchukiza mwingine.
Kitu ambacho baba yako nimefanikiwa, nilijaribu kumuabudu Mungu na mimi mwenyewe. Hiyo ndio nguzo ya kuwa wewe kama wewe na kuwa na furaha katika maisha.
Kwa kuwa wewe sio mkubwa kuliko mwingine, basi wewe sio mdogo kuliko wengine vilevile. Usiache ukweli huu uondoke moyoni mwako. Ni njia ya utambulisho wako wa wewe kama wewe. Mungu pekee ndiye anastahili kuabudiwa na yeye hataki tuwaabudu binadamu
Hakuna mtu ambaye atapinga kuwa wewe ni mzuri tena ule uliopitiliza, lakini tafadhali sana usiutumie uzuri wako kama biashara kwa kulala na kila mwanaume aliye na pesa.
Labda nikuulize tu, je kama ungekuwa mlemavu ungeutumia mwili wako kwa biashara ya kingono?
Mama yako amekuzaa ukiwa mzuri, uzuri wako ni chombo cha kukutambulisha wewe kama wewe, uzuri wako ukawe sifa kwa mwenyezi Mungu, ukawe na siha njema kwa kila mtu na watu watakujaji kutokana na tabia zako.
Kamwe usishindane na mwanaume, usiungane na makundi ya wanawake ambao kampeni zao ni kuwapanda kichwani wanaume, Mwenyezi Mungu hakukuumba hivyo.
Nguvu ya ushawishi wa mwanamke ilionekana tokea enzi za Adam na Eva katika bustani ya Edeni. Na itaendelea kukua kadiri nyakati za ulimwengu zitakavyosonga.
Kwa kujua busara hii, ukatumie vyema nguvu yako ya ushawishi kwa busara zaidi, usiende kutumia nguvu hii kwa kujiweka katika kutaka mafanikio ya kirahisi rahisi na kupata pesa kwa njia za kirahisi pasina kutumia akili.
Ninajua utakutana ma mwanaume atakayekupenda, atakuwa mwema kwako, atakuwa rafiki yako na atakuheshimu. Atakulinda na kukuweka karibu mno kwake.
Lakini mwanaume huyo hatakuwa amekamilika kwa asilimia mia moja ndio maana umeumbwa wewe kwa ajili ya kumkamilisha.
Kama utaweza kumkamilisha, kama nawe utaweza kumpenda na kunyenyekea kwake atakuwa mwanaume mwenye furaha siku zote na hilo halitapita bure.
Nataka kuzungumzia kuhusu Mapenzi, kuhusu maisha, kuhusu maumivu, kuhusu kifo, kuhusu Mungu na mengineyo lakini ooops, bado hata hujazaliwa. Hata hivyo ukayatekeleze hayo machache niliyokueleza
Nakupenda sana binti yangu.
Ni mimi baba yako.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.