Vitu 7 ambavyo huvijui kuhusu mwili wako


1. kiasi cha mate mdomoni mwako
Mate hutengenezwa na tezi mdomoni mwako ili kufanya mdomo wako uendelee kuwa na unyevu na kufanya meno yako yake safi na pia husaidia kulainisha chakula unachokula, bila mate tusingeweza kula chakula.
Mwili wa binadamu hutengeneza mate kwa kiwango cha mililita 30 kwa saa moja. mate hutengenezwa zaidi wakati wa kula na kidogo wakati wa kulala.
kiasi hiki cha mate ni sawa na chupa moja ya wine kila siku na kwa wastani wa maisha yote, mwili wa binadamu hutengeneza mate kiwango cha kujaza swimming pools mbili.
2. umbo la pekee la sikio.
Inafahamika kuwa alama za vidole yaani finger prints ndizo alama za pekee kwenye mwili ya binadamu yaani kila binadamu ana fingerprints za pekee ambazo hazifanani na za mtu mwingine yeyote.
Sasa kuna hii ambayo yawezekana hujawahi kuisikia, ambayo ni kwamba, masikio pia yana umbo la pekee tofauti kwa kila binadamu.
Umbo la sikio linatajwa kuwa sawa au bora zaidi ya njia nyingine za kutambua uso wa binadamu.
Wataalamu wamegundua kuwa, kutumia masikio kuwatambua watu ni njia ambayo ina usahihi wa asilimia 99.6.
3. aina mbalimbali za jasho
Mwili wa binadamu una tezi za jasho zaidi ya milioni 4 lakini mwili hutengeneza aina mbili tu za jasho.
Mwili huanza kutengeneza jasho kutokana na joto, homone, hisia na mazoezi.
Tezi nyingi za jasho kwenye mwili ni zinazojulikana kama eccrine ambazo huzalisha jasho lisilotoa harufu yaani ni kama jasho linalotoka kwenye mikono.
Tezi aina ya pili ni za aina ya appocrine ambazo ndizo huzalisha jasho linalotoa harufu. jasho hili linavyotengenezwa na mwili huwa na mafuta mafuta na linapokutana na bakteria ambao wako juu ya mwili wa binadamu ndipo harufu mbaya inapotokea.
4. Pua ndio kiungo nyeti zaidi kwenye mwili wa binadamu
Wanasayansi wa chuo kikuu cha Rockefeller na Taasisi ya tiba ya the howard hugges wamegundua kuwa binadamu anaweza kutofautisha takriban harufu trilioni moja.
Pia wanasayansi hawa wameeleza kuwa wanawake hunusa haraza zaidi kuliko wanaume.
5. ubongo wa binadamu hauhisi maumivu
Ukijichoma au kujikata na kitu chenye ncha kali lazima utasikia maumivu muda huo huo, hii ni kwasababu ubongo kupitia uti wa mgongo huujulisha mwili kuwa umeumia. Hii haina maana kwamba ni ubongo ndio umeumia.
Na hii ni kwasababu ubongo hauna vipokezi vya maumivu, kichwa kikikuuma sio kwamba ubongo ndio unauma bali ni utando wa kinga yaani protective membrane ambao umezunguka ubongo.
Kuumwa kwa kichwa kunasababishwa na kemikali inayotolewa na ubongo ambayo huamsha vipokezi vya maumivu na ndipo hufanya kichwa kuuma.
6. ukuaji wa nywele
Wataalamu wanaeleza kuwa binadamu wa kawaida huwa na matundu ya nywele 100,000 na kila moja huweza kuotesha nywele 20 katika kipindi chote cha maisha ya mtu.
Nywele huoza kwa kiwango kidogo sana, lakini pia seli za nywele ndizo seli zinazokuwa haraka zaidi na kushika namba mbili baada ya seli za utumbo ambazo ndizo za kwanza.
7. Asidi ya tumbo inaweza kuyeyusha metali
Inajulikana kwamba asidi inayopatikana kwenye tumbo la binadamu husaidia katika kuyeyusha chakula na kulinda tumbo dhidi ya maambukizi mbalimbali tukila chakula.
Asidi hii inaelezwa kuwa imeundwa na asidi nyingine za hydrocloric, potassium na sodium. mchanganyiko wa kemikali hizi ambao unafananishwa na asidi ya betri unaelezwa kuwa mkali kiasi cha kuwa na uwezo wa kuyeyusha kiwembe.
Hata hivyo asidi hii haileti madhara kwa tumbo la binadamu kwani seli za tumboni hujitengeneza upya haraka kila baada ya siku tatu hadi nne.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.