Hatua Ya 5 za Mfanyabiashara Mdogo Kuelekea Kwenye Mafanikio

Image result for MFANYABIASHARANaamini unaendelea vizuri.
Je, umeweza kufanyia kazi mambo uliyojifunza kutoka email zilizopita? Kama ndiyo, naomba nishirikishe matokeo baada ya kuanza kutumia mbinu ulizojifunza. Kama bado, nieleze kitu gani kinachokukwamisha usitekeleze kwa vitendo mafunzo uliyopata kupitia email.
Leo naongelea mfanyabiashara ambayo yupo hatua ya 5. Kama nilivyokueleza awali, hatua hii, biashara yako inatengeneza kipato kikubwa kinachokidhi mahitaji yako na kingine kubaki kama akiba. Kiasi kinachobaki kinaweza kuwekweza katika biashara yako, au biashara nyingine ambayo umefanyia utafiti wa kutosha na unaamini ukiwekeza huko, itazaa na kukua.
Kama upo hatua hii, basi unatakiwa kufanya yafuatayo kuweza kuipeleka biashara yako hatua inayofuata, hatua ya 6:
  1. Jenga mfumo wa biashara yako, kusudi utumie muda mfupi kwenye biashara. Pia uifundishe kujiendesha, maana kuna wakati utaihitaji ijiendeshe yenyewe wakati wewe haupo.
  2. Ukishajenga mfumo, basi ni muhimu kuhakikisha unawapa haki watumiaji wa bidhaa yako kuhakikisha wanaweza kupata bidhaa/huduma zako kule walipo. Ukishakuwa na mfumo, ni rahisi kuiwezesha biashara yako kutoa huduma nzuri na inayotarajiwa na wateja wako. Kwa kufanya hivyo, pato la biashara linaongezeka, pia pato lako binafsi linaongezeka.
Je, ni mifumo ipi unahitaji kuijenga?
Kwa mfanyabiashara mdogo mwenye wafanyakazi wasiozidi mia, nashauri ajenge mfumo wenye mifumo ifuatayo, 1) pesa,2)  wateja, 3) mwenye biashara, 4) wafanyakazi na wadau wengine muhimu katika biashara yako. Ukiweza kutengeneza mfumo utakaogusa vitu hivyo 4, basi elewa umefanikiwa na kuna uwezekano mkubwa ukaipaisha biashara yako.
Kukuweza kukusaidia kusudi uanze kujenga mfumo wa biashara yako, naona bora nikueleze kwa undani kuhusu mfumo wa pesa. Endelea kujifunza zaidi kuhusu mfumo huu.
Mfumo wa PESA:  ni muhimu sana kwa biashara yeyote kuanza na mfumo wa kusimamia pesa zinazoingiz, zinazotoka na zinazoingia. Pesa ndo moyo wa biashara, usipojua mwenendo wa pesa katika biashara yao, basi ujue hutoweza kupata maendeleo endelevu. Kuna uwezekano utatengeneza pesa, lakini ukajikuta huoni tena pesa katika biashara yako.
Kuhakikisha una mfumo mzuri utakaosimamia mwenendo mzima wa biashara yako, nakushauri ufanye yafuatayo.
Kuwa na mfumo wa kumbukumbu kwa ajili ya kurekodi shughuli za kifedha katika biashara yako. Kama unakumbuka hapo nyuma, nilishauri uwe na kumbukumbu zifuatazo kwa kuanzia:
  1. Taslimu
  2. Mauzo
  3. Manunuzi
  4. Matumizi
  5. Maujudi (stock)
  6. Wadaiwa
  7. Wadai
Mfumo huu ni muhimu sana kwa kuanzia. Bila mfumo wa utunzaji kumbukumbu, kuna uwezekanao mkubwa ukapoteza mali.
Mfumo mwingine muhimu sana kwako, ni ule wa kutengeneza ripoti kila mwezi. Kuna ripoti kuu tatu kwa mfanyabiashara mdogo. Nazo ni:
  1. Ripoti ya fauda au hasara
  2. Ripoti ya mtiririko wa taslimu
  3. Ripoti ya mizania
Ingawa unaweza kuandaa ripoti nyingi zaidi ya hizi, nashauri kwa mfanyabiashara mdogo, ahakikishe anatengeneza ripoti hizi kila mwezi bila kukosa. Ukiwa na muda, unaweza ukawa unatengeneza kila wiki, au hata kila siku. Nakuomba tafadhali sana hakikisha unafanyia kazi hili.
Tengeneza kanuni za usimamizi wa pesa zako zinavyoingia, zinavyotoka, unapoamua kuwekeza, nk. Mfano wa kanuni hizi waweza kuwa,
  1.  Pesa yote ya biashara itawekwa benki kabla haijatumika
  2. Nitatenga 5% ya mauzo na kuiweka benki kama akiba ya uwekezaji
  3. Mauzo yangu yote yatakuwa ni cash kupitia cash, benki na simu
Kwa faida ya biashara yako, orodhesha kanuni unazotumia, na kama hujatengeneza, basi ziandike sasa. Kanuni hizi zinatakiwa ziwe ziseme vitu utakavyokuwa ukifanya kuhusiana na pesa, na zile utaamua usizifanye.
Andika hatua ya safari za pesa Hatua pesa inavyoingia katika biashara na inavyotoka. Tuchukulie mfano wa mgahawa:
 Hatua 1: Mteja anatoa oda kwa muhudumu
Hatua 2: Mteja anapewa bill baada ya kumaliza kula
Hatua 3: Muhudumu anapokea cash, anatoa risiti na kurudisha chenji sahihi.
Hatua 3: Muhudumu namuomba mteja ahesabu pesa mbele yake kabla ya kuondoka.
Hatua 4: Muhudumu anampatia pesa cashier,
Hatua 5: nk.
Unapoandika hatua hizi, hakikisha unaandika hadi safari ya mwisho ya pesa. Na katika kila hatua huwa kuna checklist, fomu mbalimbali, na sampuli zinazowezesha hatua hizo kufanyika vyema na kwa ufanisi. Pia katika hatua amua aina gani ya kumbukumbu na ripoti zitahitajika kwa ajili ya kiongozi wa biashara. Ukiweza kufanikiwa kujenga mfumo katika hatua hii ya 5, basi biashara yako itakuwa imepata nafasi kubwa sana ya kuelekea kujiendesha yenyewe, na kukupa mafanikio unayoyataka.
Naomba niishie hapa leo.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.