Daraja la Dumila lasombwa na maji baadhi ya majengo ya Shule yafunikwa.
Habari
zilizopatikana mchana huu zinasema kuwa Daraja la Dumila lililopo
mkoani Morogoro ambalo ni barabara ya Dodoma – Morogoro limekatika na
magari hayapiti baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya magari yatokayo upande wa Dodoma na Morogoro yameamua
kugeuza na kurudi yalipotokea maana hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo.
Kutokana na mvua hiyo madarasa katika Shule ya Msingi Magole, Dumila,
Morogoro nayo yamefunikwa na maji na wanafunzi kuamua kujiokoa kwa
kupita madirishani. Mpaka sasa hali bado si nzuri eneo hilo la Dumila
wilayani Mvomero.
Leave a Comment