Dk. Seif Rashidi:JITOKEZENI KUPIMA UGONJWA WA UKOMA
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashidi amitaka jamiikuwahi
mapema katika vituo vya afya ili kuweza kupata uchunguzi pindi
wanapoona mabaka ya aina yoyote katika ngozi ya mwili ili kuweza
kupata tiba sahihi ya ugonjwa wa ukoma na kuepusha ulemavu usio wa
lazima.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri huyo alipokuwa akitoa tamko kuhusu Siku ya
Ukoma Duniani itakayoadhimishwa nchini kila mkoa Januari 26, mwaka huu
kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo leo jijini Dares Salaam.
Alisema Tanzania ni miongoni wa nchi 17 duniani ambazo zina viwango bado zina viwango vya juu wa ugonjwa wa ukoma.
“Athari
kuu ya ugonjwa wa ukoma ni ulemavu wa kudumu . Ulemavu unatokana na
kuchelewa kwa uchunguzi na matibabu sahihi . Tujenge tabia ya kuchunguza
miili yetu na pale tunapoona mabadiliko yoyote yanajitokeza twende
mapema katika vituo vyetu vya huduma kuchunguzwa ili tupate ushauri
na matibabau stahili,” alisema Dk. Rashidi.
Dk.
Rashidi asilimia 11 ya wagonjwa wapya wa ukoma wanaojiotokeza
katika vituo vyetu kwa ajili ya uchunguzi na kuanza matibabu wanakuwa
tayari wana ulemavu wa kudumu .
Aliongeza kuwa ugonjwa huo hutibiwa na dawa mseto (Multi drug theray au MDT) na zipo za kutosha.
Alisema
takwimu za hapa nchini kwa miaka mitano iliyopita zinaonesha kuwa
idadi ya wagonjwa wapya wa ukoma inazidi kupungua kutoka 3,248 mnamo
mwaka 2008 hadi 2,548 kwa mwak 2012 .
Aliongeza
kuwa bado kuna wilaya 15 mabazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza
ugonjwa huo cha chini mgonjwa 1 kati ya watu 10,000 katika jamii husika.
Alizitaja wilaya wilaya hizo ni Liwale ,Nachingwea,Mkinga,Pangani,
Muheza, Rwangwa, Mvomero, Kilwa, Msasi, Chato, Nanyumbu,Lindi
Kisarawe,Newala na Songea.
Alizitaka
halimashauri mabazo zina wagonjwa wengi, kutenga fedha kwa jili ya
kuhamasisha wanachi kutambua dalili za wali za ukoma ili kuwahi
matibabu na kuzuia maambukizi mapya .
Dk.
Changamoto wanazokabiliana katika kupambana na ugonjwa huo, watumishi
wa afya kutambua kwa urahisi ugonjwa huo, jamii kuendelea kushikilia
imani potofu na kuchelewa kujitokeza kupata matibabu hadi wanapopata
ulemavu.
Ugonjwa huo ni wa kuambukia unaoletwa na vimelea hai na unasambazwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mgonjwa kwenda k wa mtu ambaye hana vimelea hivyo.
Leave a Comment