MKUU WA WILAYA AKAGUA MAONYESHO YA UJASIRIAMALI YA VIJANA WA MOROGORO
Mkuu
wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili kukagua maonyesho ya vijana wajasiriamali ya mkoa
wa morogoro akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
iliyoandaa maonyeshi hayo Ndugu Jackson Audiface. Maonyesho hayo ambayo
yapo katika mpango wa kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana ujulikanao
kama Tanzania Youth Entrepreneurship Programme (TAYEP) ambao upo chini
ya kampuni ya AJ IT Development Company Ltd.
Mkuu
wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akikagua baadhi ya bidhaa
zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka mkoa wa morogoro. baadhi ya
vijana hao kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Chuo kikuu Mzumbe, Chuo
kikuu cha kiislaam Morogoro. Lengo la maonyesho hayo ni kuzitangaza na
kuzitafutia masoko kazi za vijana wajasiriamali.
Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi katika meza kuu akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni iliyoandaa maonyeshi hayo Ndugu Jackson Audiface (aliyevaa
shati jeupe) pamoja na mwenyekiti wa kikundi cha vijana wajasiriamali
wa morogoro kijulikanacho kama MOMUYO ndugu Alexander Jokonia (wa pili
kutoka kulia) pamoja na afisa tarafa wa manispaa ya morogoro Mh Pakala
Pakala (wa mwisho kulia).
Baadhi
ya washiriki mbalimbali kutoka vyuo na vikundi mbalimbali vya
wajasiriamali kutoka mkoani morogoro walioshiriki katika maonyesho hayo .
Mwakilishhi
wa serikali ya wanafunzi kutoka chuo kikuu Mzumbe Ndugu Norbert
Kabendera akitoa neno la shukrani wakati wa maonyesho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akizindua tovuti ijulikanayo kama MATUKIO NA VIJANA itakayokua
ikiripoti masuala ya kijamii hususani masuala ya vijana, akisaidiwa na
Mkurugenzi wa Utawala na Mipango wa kampuni ya AJ IT Development Company
Ndugu Fasali Mwenzegule. Pamoja na uzinduzi huo Mkuu wa wilaya
alizindua mitandao mbalimbali ya kijamii itakayotumika katika mpango huu
ikiwemo akaunti katika Instagram (@youth_entrepreneurship), twitter
(@youth_entrepreneurs) na facebook (Tanzania-YOUTH-Enterprenuership).
Mkuu
wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akitoa hotuba mara baada ya
kukagua maonyesho hayo ambapo aliomba taasisi za fedha kupunguza riba
kubwa za mikopo hasa kwa vijana wanaojiajiri pamoja na hilo aliomba
makampuni mengi kujitokeza kuwezesha mpango kufanyika nchi nzima ili
uweze kuwafikia vijana wengi zaidi Tanzania.
HABARI KAMILI
Tanzania
Youth Entrepreneurship Programme (TAYEP) ni mpango ulianzishwa na
kampuni ya AJ IT Development Company kwa lengo la kuwasaidi vijana ambao
hawana ajira kuweza kujiajiri kwa kuwa wajasiriamali.
Mpango huu
uliobuniwa mwaka 2013 umewawezesha vijana 50 kutoka mikoa ya Arusha na
morogoro kujiajiri kwa njia ya kilimo, Utalii na ubunifu wa kazi za
mikono. Lengo la mpango huu ni kutangaza na kuzitafutia masoko kazi za
wajasiriamali, kutoa elimu kuhusu ujasiriamali kwa vijana ambao
hawajiajiri, kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na
vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Mkakati
iliyowekwa na kampuni hiyo kwenye mpango huu ni kupeleka maonyesho haya
mikoa yote Tanzania kwa lengo la kuwafikia vijana wengi zaidi ambao
bado hawajiajiri.
Changamoto
kubwa zinazoukabili mradi huu ni ukosefu wa rasilimali fedha ambao
unasababisha vijana wengi kukosa fursa hii, tunawaomba wadau mbalimbali
wa vijana kujitokeza kusaidia mradi huu kuwafikia vijana wengi zaidi ili
kuwasaidi vijana wengi kupata ajira na nchi iweze kupiga hatua kubwa
kwenye maendeleo na kutimiza kauli mbiu ya matokeo makubwa sasa yaani
“BIG RESULT NOW”.
Leave a Comment