TAARIFA YA HABARI YA PLANET FM
HII HAPA
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanikiwa
kukusanya sh. bilioni 83.4 kufikia mwaka 2013/2014 ambazo zinatokana na
shughuli mbalimbali zilizofanywa na Idara ya Uhamiaji.
..............................
Serikali ya Tanzania, kwakushirikiana na
mashirika manne ya kimataifa leo
wamezindua mpango wa pamoja wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto nchini.
......................................
Serikali imefanikiwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni
moja na milioni 750, kama fidia kwa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mara baada
ya kuchukua mradi wa Halmashauri hiyo, ujulikao kama Laki Laki kwa ajili ya
kujenga miji ya kisasa katika maeneo hayo.
KIMATAIFA
Mataifa ya nchi za Afrika Mashariki yameidhinisha kupelekwa kwa kikosi
cha wanajeshi 5,500 nchini Sudan Kusini ili kumaliza mgogoro wa kisiasa ambao
umekuwa ukiendelea kwa wiki kadhaa nchini humo.
..............................
Watu
watatu wameripotiwa kuuawa katika wimbi jipya la maandamano ya kuipinga
serikali ya Ukraine, tukio ambalo limechochewa na mgogoro wa kisiasa wa nchi
hiyo, uliodumu kwa miezi miwili sasa.
.........................
Shirika la kimataifa la kuhudumia Watoto la UNICEF, limeanza
kuandaa kampeni ya chanjo kwa Watoto zaidi ya milioni 1na laki 6 ili kupambana
na ugonjwa wa Surua uliojitokeza nchini Guinea.
.... MWISHO....
Leave a Comment