PENGO ANAUMWA
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (70) ni mgonjwa, imetangazwa.
Taarifa ya kuugua kwa Kardinali Pengo, kiongozi wa kiroho anayeaminika
kwa kukosoa uovu unaofanywa kwenye jamii, imetangazwa na Askofu Msaidizi
wa kanisa hilo jimboni humo, Mhashamu Titus Mdoe.
Mdoe, alitoa taarifa hiyo wakati wa misa takatifu iliyofanyika jana kwenye kigango cha Nzasa, parokia ya Temboni jimboni humo.
Misa hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi na huduma za kiroho kwa kigango hicho kinachotarajiwa kupandishwa hadi ili kiwe parokia.
Misa hiyo ilikuwa mahususi kwa ajili ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi na huduma za kiroho kwa kigango hicho kinachotarajiwa kupandishwa hadi ili kiwe parokia.
Mhashamu Mdoe hakutaja ugonjwa unamsumbua Kardinali Pengo, lakini
aliwataka Wakatoliki na watu wenye mapenzi mema, kuendelea kumuombea ili
apate nafuu.
Alisema ugonjwa wa Kardinali Pengo unaweza kuchangiwa pia na hali ya
kuelekea katika uzee, ingawa sababu hiyo haijafikia kuwa chanzo kikuu
cha kumfanya augue.
Katika hatua nyingine, Askofu Mdoe alisema utumishi wa umma ulio bora
unapaswa kuelekezwa katika kutatua umasikini na kero zinazoikabili
jamii, hivyo kufikia tarajio la kuwa maisha bora.
Pia alikosoa tabia ya baadhi ya viongozi hususani watawala, kupiga picha
zenye mwelekeo wa kushiriki na kutatua kero za jamii, huku lengo likiwa
ni kupata nafasi kwenye vyombo vya habari.
Alisema miaka 52 ya Uhuru ilitosha kwa kutatua umasikini na kero nyingine zinazoikabili nchi.
Badala yake, alisema walio katika dhamana ya kufanikisha azma hiyo,
wameshindwa kufikisha tumaini la maendeleo kwa wananchi hasa wa
vijijini, licha ya ukweli kwamba maendeleo mijini yanakua kwa kasi.
Mhashamu Mdoe, alisema watu kama maafisa kilimo ambao damu zao zipo kwa
kuwatumikia watu, hawapaswi kukaa maofisini wakiwa wamevaa suti, bali
kuhakikisha wantekeleza wajibu wa kuwahudumia wakulima.
Alisema kuna maeneo mengi ya nchi yasiyofikiwa na mahitaji muhimu kwa
jamii kama umeme, maji, afya na elimu bora, hivyo kuwafanya wasinufaike
na matunda yanayotokana na Uhuru na rasilimali za nchi.
Leave a Comment