BREAKING NEWS;
MMILIKI WA MAN UNITED AFARIKI DUNIA
BILIONEA
Malcolm Glazer, aliyeshinda tenda ya utata ya kuichukua Manchester
United mwaka 2005, amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 85.
Mfanyabiashara
huyo wa Marekani atakumbukwa kama bilionea wa Florida aliyeichukua
kuimiliki binafsi United miaka tisa iliyopita na kuwekeza zaidi ya Pauni
Milioni 500.
Glazer mkubwa amekuwa mgonjwa kwa muda sasa na kuwaachia shughuli za uendeshaji wa United watoto wake wa kiume, Joel na Avram. 

Mmiliki: Malcolm Glazer amefariki akiwa na umri wa miaka 85
Msemaji wa United amesema: "Fikra za kila mmoja katika United zipo kwa familia usiku huu,".
Familia
ya Glazer bado wanamiliki Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu
ya Marekani waliyoinunua mwaka 1995. Na kwenye tovuti ya Bucs, ambako
zimetangazwa habari za kifo cha Glazer.
Wakati wa umiliki wa Glazer, United imeweza kushinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Glazer ameacha mke, Linda waliyefunga naye ndoa mwaka 1961 na watoto na watoto sita, Avram, Kevin, Bryan, Joel, Darcie na Edward.

Leave a Comment