Watu watatu wamefikishwa katika mahakama ya
hakimu mkazi mkoani morogoro, kwa kosa la kula njama na kumfanyia ukatili mtoto
Nasra Rashidi mwenye umri wa miaka 4 mkazi wa Kiwanja cha ndege Manispaa ya
Morogoro.
Akisoma mashitaka hayo, msoma mashitaka wa
mahakama hiyo Bi. Anganile Msyani amesema watuhumiwa wametenda makosa kati ya mwezi
Desemba mwaka 2010 na May 2014, ambapo walimuweka mtoto huyo ndani ya boksi kwa
muda wa miaka minne kitendo kilichosababisha utapiamlo, kuvunjika kwa miguu na
mikono pamoja na udhaifu wa mwili kwa mtoto huyo.
Aidha, watuhumiwa hao ni Mariam Saidi mwenye
umri wa miaka 38 kabila Myao, Mtonga Omary miaka 30 Mluguru wote wakazi wa
Kiwanja cha ndege na Rashidi Mvungi miaka 47 Afisa Elimu Morogoro vijijini
mkazi wa Lukobe wametenda makosa hayo yaliyopo kwenye kesi namba 79 ya mwaka
2014.
Pia imeelezwa kuwa, upelelezi umekamilika
na dhamana iko wazi kwa kila mshitakiwa, kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa
pamoja na shilingi milioni tano za kitanzania kwa kila mmoja, ambapo kesi hiyo
itatajwa tena mnamo tarehe 9 mwezi wa 6 mwaka huu.
Leave a Comment