BREAKING NEW:
WAMBURA BASI TENA SIMBA, KAMATI YA TFF YAMTUPA
Taarifa zinaeleza Michael Richard Wambura amepigwa chini
na kamati ya rufaa ya TFF.
Kamati hiyo imeungana na kamati ya uchaguzi ya Simba chini
ya Dokta Damas Daniel Ndumbaro ‘DDN’ ambayo ilimpiga chini Wambura kugombea
Simba baada ya kubaini alipiga kampeni kabla ya muda.
Rufaa yake aliyokata katika kamati ya rufaa ya TFF
ilisikilizwa leo kwenye hoteli ya Courtyard jijini Dar.
Leave a Comment