Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mstaafu Josephat Mwingira azikwa
Na Insp. Deodatus Kazinja,PHQ
Aliyewahi
kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Mzee Josephat
Mwingira aliyefariki tarehe 09 Juni, 2014 na kuzikwa tarehe 12 Juni,2014
katika Makaburi ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam
kwa heshima zote za kijeshi.
Marehemu
Mwingira aliajiriwa katika Jeshi la Magereza tarehe 11 January 1956
ambapo alianzia kazi katika Gereza Kuu Butimba la Jijini Mwanza na
maeneo mengine mengi nchini hadi alipo staafu kwa mujibu wa sheria
tarehe 01 Julai, 1990 akiwa amelitumikia Jeshi la Magereza kwa miaka 33.
Hayati
Mwingira mbali na kuwa kiongozi katika Jeshi la Magereza lakini pia
alikuwa kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alishika nyadhifa
kadhaa enzi za siasa majeshi.
Kamishana
Jenerali wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya watumishi wote wa Jeshi la
Magereza anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafika kwa msiba huu
mzito.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiingiza mwili wa Marehemu
na kuuingiza nyumbani kwake baada ya kutoka “mortuary”.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa
aliyemwakilisha Kamishna Jenerali wa Magereza akitoa salaam za mwisho
kwa marehemu.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mmeta Manyara
(wa kwanza kushoto) akitoa heshma zake kwa marehemu
Baadhi
ya wastaafu wa Jeshi la Magereza wakitoa salamu za mwisho kwa marehemu
Mwingira (wa kwanza mbele) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Saimon
Mwanguku, wa pili ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Alhaji Jumanne
Mangara. Wawili hao walifanya kazi kwa karibu sana na Marehemu Mwingira
enzi za uhai wake.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioko kazini na wastaafu
kwa pamoja wakijumuika na wananchi wa kijiji cha Kilongawima Kata ya
Kunduchi jijini Dar es salaam waliokusanyika na wanafamilia katika
safari ya mwisho ya Marehemu Mwingira
Askari
wa vyeo mbalimbali wakijumuika na wananchi wa kijiji cha Kilongawima
Kata ya Kunduchi jijini Dar es salaam waliokusanyika na wanafamilia
katika safari ya mwisho ya Marehemu Mwingira.
Mwenyekiti
wa CUF Taifa na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Prof. Ibrahim Lipumba
(wa pili kuli waliokaa kwenye viti) alikuwa miongoni mwa wananchi wa
eneo la Kiliongawima Kata ya Kunduchi Jijini Dar es salaam katika
kuifariji familia katika msiba huo mzito.
Mbunge
wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi (mwenye nguo nyeusi) alikuwa
miongoni mwa wananchi wa eneo la Kiliongawima Kata ya Kunduchi Jijini
Dar es salaam katika kuifariji familia katika msiba huo mzito. Marehemu
Mwingira ni mzaliwa kijiji cha Mbaha Kata ya Lituhi Wilaya ya Mbinga
Mkoani Ruvuma.
Ibada
ya mwisho makaburini iliyoongozwa na Padre Paul Chiwangu kutoka Baraza
la Maaskofu Katoliki Tanzania pamoja na Paroko wa Parokia ya Mtongani
Padri Paul Malewa.
Baadhi
ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza walioshirikia katika kuandaa
na kufanikisha paredi la mazishi ya Marehemu Mwingira.
Baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Mwingira wakiweka mashada ya maua.
Picha zote na Insp. Deodatus Kazinja, Makao Makuu ya Magereza
Leave a Comment