Kenyatta:Mauaji yalishinikizwa kisiasa
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
amesema kuwa mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni, Pwani ya Kenya
hayakufanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja siku moja baada ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketo walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa lkuna baadhib ya wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa jamii.
Leave a Comment