AlShabab yaua mama kwa kutofunga mtandio
Wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab wamempiga mwanamke mmoja risasi na kumuua kwa kukosa kujifunga mtandio kichwani.
Jamaa za mwanamke huyo mwenyeji wa mji wa
Hosingow kusini mwa Somalia wanasema mwanamke huyo alikataa kujifunika kitambaa kichwani kuambatana na sheria za dini ya kislamu.
''alikuwa ameonywa ajisitiri lakini wapiganaji hao waliporejea wakashikwa na hasira walipopata kuwa hakuwa amejifunika na hivyo wakampiga risasi''.
Jamaa zake wameiambia BBC kuwa Ruqiya Farah Yarow alikuwa amewafokea wapiganaji hao akiwataka waondoke kwake na kusema kuwa angejisitiri baadaye.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo amekanusha kuwa ni wao waliomuua mwanamke huyo .
Msemaji huyo anasema kuwa licha ya kudhibiti maeneo makubwa nchini humo kundi hilo bado halijatoa maelezo ya vipi wanawake wanastahili kujisitiri.
Leave a Comment