Kocha wa Brazil amgeukia mwanasaikolojia
Scolari amefanya hivyo mara baada ya kikosi hicho kumwaga machozi katika hatua ya mikwaju ya penati kwenye mechi dhidi ya Chile katika hatua ya 16 bora ambako Brazil waliibuka washindi.
Wenyeji hao waliibuka na ushindi wa penati 3-2 na ilionekana wachezaji wengi wa kikosi hicho cha Selecao walikuwa wakibubujikwa na machozi wakati walipo kuwa wakishangilia ushindi wao katika uwanja wa Estadio Mineirao.
Mshambuliaji wa Brazil Neymer alikuwa miongoni wachezaji waliokuwa wakitoa machozi kwa hisia kali.
”Mchezo kati yetu na Chile ulikuwa wa kusisimua karibu kwa kila mmoja wetu.”
“Lakini hilo halimanishi kikosi chetu kimetawaliwa na presha kubwa pamoja na uwoga wingi.”
Wenyeji hao wanakabiliwa na presha kubwa yakulibakiza Kombe hilo la Dunia katika ardhi ya nyumbani na watarajia kukabiliana na mtihani mgumu pale watakapokutana uso kwa uso na Colombia katika hatua ya robo fainali mchezo utakaofanyika siku ya Ijumaa.
Neymar ndiye mchezaji wao tegemezi na tayari ameshakifungia kikosi chake mara nne katika michuano hiyo mpaka sasa.
”Sijisiki kuelemewa na majukumu ya kikosi changu kwa sababu wachezaji wote tunashirikiana katika kuhakikisha ushindi unapatikana.”
“Ninao wachezaji wenzangu wanaonisaidia. Kuna mabeki wanaokaba mipira vizuri nakuimiliki,kunawanao toa pasi, wengine wanafunga magoli.”
Sisi tunacheza kama timu na hatutegemei uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.
“Kitu cha muhimu kwetu ni kuhakikisha Kombe la Dunia linabaki katika ardhi ya nyumbani”, alieleza Neymar.
Leave a Comment