Alichopost Luis Suarez akiomba msamaha – Chiellini amjibu
Akitumia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Luis Suarez aliandika ujumbe mfupi akiomba msamaha kwa Giorgio Chiellini na wanafamilia wa soka ulimwenguni kote kutokana na kitendo alichofanya.
Suarez ambaye aliadhibiwa kifungo cha mechi tisa zinazosimamiwa na FIFA pamoja na kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 4, amekiri makosa yake na kuahaidi tukio kama lile halitojirudia tena.
Muda mfupi baada ya Suarez kutuma ujumbe huo – Chiellini alimjibu na kumwambia amemsamehe na angependa FIFA impunguzie adhabu.
Leave a Comment