MAREKANI YAPIGWA 2-1 NA UBELGIJI, LAKINI KIPA WAO AANDIKA BONGE LA REKODI..
Kijana wa kazi: Howard aliokoa michomo mingi zaidi ukilinganisha na kipa mwenzake wa Ubelgiji, Thibaut Courtois
Howard akijitanua na kuokoa mpira uliopigwa na nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany
Kwa kuokoa michomo 15, kipa huyo wa
Everton ameandika rekodi mpya ya kombe la dunia tangu takwimu kama hizo
zipatikane mwaka 1966 ambapo kipa wa Peru, Ramon
Quiroga aliokoa michomo 13 mwaka 1978 dhidi ya Uholanzi.
Kiwango cha jana cha Howard ndio bora
zaidi kuwahi kutokea katika timu ya Marekani tangu Sylvester Stallone
afanye hivyo mwaka 1981.
Leave a Comment