MSICHANA AUWAWA KINYAMA DODOMA
Kinamama walio karibu na familia ya marehemu
Isabela Andrew aliyebakwa hadi kufa wakiangua kilio baada ya kushuhudia mahali
mwili wake ulipokutwa huko Area C mjini Dodoma jana.Mwili wa msichana huyo
ulikutwa ukiwa umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini
na paparazi alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji
mashuhuda wa tukio hilo.
Dodoma. Mfanyakazi wa ndani, Isabella Andrew (18),
amefariki dunia na kifo chake kikidaiwa kusababishwa na kubakwa na watu
wasiojulikana.
Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa umeharibika
katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na mwandishi wetu
alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji mashuhuda wa
tukio hilo.Mkazi wa Mtaa wa Kiwanja cha Ndege, Jackson Coy aliyekuwa akiishi na
binti huyo alisema msichana huyo alipotea tangu Jumamosi iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime,
alisema mwili huo uliokotwa jana saa mbili asubuhi na kwamba polisi wanaendelea
na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.Mwili huo ulibainika baada ya mama
mmoja, Rehema Msambile kufika katika pagale hilo alipokuwa akifuatilia nyendo
za mtoto wake ambaye juzi alipigwa kwa tabia ya utoro shuleni.“Niliamua leo
(jana) kumfuatilia, nikaanza katika mapagale.Nilipofika hapa ndipo nikaona
mwili wa marehemu ikabidi nimuite jirani hapo aje aone,” alisema.
Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Henry Kandenga
alisema mazingira yanaonyesha kuwa binti huyo alibakwa kwa sababu walikuta nguo
za ndani zikiwa pembeni.“Hakuna yowe iliyosikika kwamba kuna mtu anauawa
ukizingatia kwamba nyumba ziko jirani na hata nyumba aliyokuwa akiishi ni
jirani na mahali alipokutwa,” alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Dodoma.
Leave a Comment