MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM MKOA WA SHINYANGA MBARONI KWA KUVUNJA VIOO VYA GARI ALILOKUWA AMEKODI NA KUGOMA KULIPA.


 JESHI la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linamshikiria Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM [UVCCM]mkoani Shinyanga Mapinduzi Mabula kwa tuhuma ya kufanya fujo na kuharibu mali.
 
Kwa mujibu wa taarifa za Polisi zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,Kihenya Kihenya,Mabul;a ambaye pia ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Shinyanga TRA amekamwatwa jana jioni.
 
Katika tukio hilo Mapinduzi alifika mjini Kahama akitokea Shinyanga na kisha kukodi taxi namba T 992 CGQ iliyokuwa ikiendeshwa na Nicholaus Bilambona ambapo alikataa kulipa hali iliyozua vuruga iliyopelekea Kiongozi huyo wa UVCCM kuvunja vioo vya gari hiyo.
 
Hata hivyo Mabula alikamatwa na Polisi na kufikishwa kituoni ambapo napo alifanya fujo akigoma kuingizwa mahabusu mpaka pale askari walipotumia nguvu ya ziada kumweka chini ya Ulinzi kwenye chumba cha kuhifadhia wahalifu.
 
Wakati leo mchana kipindi hiki kikitoka Kituo cha Polisi Kahama Mtuhumiwa alikuwa bado mahabusu huku jitihada za kumtoa kwa dhamana zilizokuwa zikifanywa na UVCCM wilaya ya Kahama zikiendelea ingawa kesho asubuhi anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake .

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.