MADHARA YA KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA
Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika. Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina....
1. KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Watu wenye pupa za kufanya
mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu
za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara
kwa mara. Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi
cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.Kukinai haraka staili za kimapenzi hujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
2. KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia ya kufanya mapenzi
mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na
msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa, na hivyo
kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la
nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani?Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake. Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi. Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.
3. KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo hutegemea
sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi,
hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa
tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako. Kama ni
mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo.
4. KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara mengine yanayoweza
kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi
za mwili. Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu
nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya
mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha. Sambamba
na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara
huwa dhaifu na wakati mwingine zinaweza zisiweze kumpa mwanamke ujauzito.
5. KUPATA MAGONJWA
Kama tulivyojifunza kuwa
watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya
mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi,
lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake
huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute
unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia
michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo
ukimwi.Baada ya kungalia madhara hayo machache ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara.
Ili kuweza kupata masomo kama haya na mengine mengi pamoja na habari za kila aina, like ukurasa wangu wa facebook Mr. Clever
Leave a Comment