BAADA YA
KUFICHAFICHA, HATIMAYE SASA MAMBO YAKO WAZI NA LUIS SUAREZ ATASAFIRI
WIKI IJAYO KWENDA KUSAINI MKATABA WA MIAKA MITANO NA BARCELONA.
KABLA YA HAPO ATAFANYIWA VIPIMO NA ZOEZI LA KUSAINI NA KUTAMBULISHWA KWA
MASHABIKI LITAFANYIKA MARA MOJA. ADA YA UHAMISHO NI KITITA KINONO CHA
PAUNI MILIONI 75.
SUAREZ MWENYE SIFA YA KUUMA WENZAKE UWANJANI, AMEONDOKA LIVERPOOL AMBAYO
IMEONYESHA ILIKUWA TAYARI KUMUACHIA BAADA YA KUMNG'ATA BEKI GIORGIO
CHIELLINI WA ITALIA KATIKA MECHI YA KOMBE LA DUNIA KATI YA URUGUAY NA
ITALIA.
BLOGI HII ILITOA PICHA YA JEZI ZA LIVERPOOL, NAMBA 9 AMBAZO ZILIKUWA
ZINAUZWA KWENYE DUKA LA KLABU HIYO, HALI AMBAYO ILIKUWA NI UTHIBITISHO,
SASA SUAREZ AMEPIGA PICHA AKIWA AMEPIGA UZI WA BARCELONA KUTHIBITISHA
HILO. |
Leave a Comment