Baba adaiwa kumbaka binti na kumpa ujauzito
Na Mwandishi wetu
SERIKALI
ya Kijiji cha Bwekela,Kitongoji cha Mwina, kata ya Igoweko,wilayani
Igunga, Mkoa wa Tabora inamtafuta mkazi mmoja wa Kijiji hicho, Kashinje
Shima kwa tuhuma za kumbaka na
kumpa mimba mtoto wake wa kike,Mbalu
Kashinde mwenye umri wa miaka 17.
Mama
mzazi wa mtoto huyo,Jeni Njiro alisema tukio hilo lilitokea
Julai,23,mwaka huu baada ya binti huyo kugundulika kuwa na ujauzito wa
miezi saba sasa.
Alisema
kabla ya kugundua kitendo hicho cha kinyama kilichokuwa kikifanywa na
mumewe, inasemekana kuwa baba wa mtoto huyo alikuwa akitumia mwanya wa
kutokuwepo nyumbani kwa mama wa mtoto na ndipo alipokuwa akifanya tendo
hilo la ndoa na mtoto wake.
Kutokana
na hofu aliyoanza kuwa nayo juu ya mwenendo wa mumewe na mtoto wake
huyo ndipo siku moja walipokuwa shambani wakiendelea na shughuli za
kuvuna mazao na mara tu mumewe alipoaga kurudi nyumbani,muda mfupi
baadaye naye alimtuma mtoto wake mkubwa wa kiume ili akafuatilie
nyumbani kupata uhakika wa kile alichokuwa akihofia.
Hata
hivyo mama huyo alisema mara baada ya mtoto wake huyo kufika nyumbani
ndipo alikuta baba yake wakifanya tendo la ndoa na mdogo wake na hivyo
kurudi shambani na kumweleza ukweli wa jambo hilo mama yake.
Ndipo
inasemekana baada ya taarifa hiyo mama yake aliamua kuita ndugu wa
pande zote mbili kwa ajili ya kuzungumzia unyama huo na alipohojiwa
katika kikao hicho cha kifamilia, alikana kuhusika na tuhuma hizo,na
baada ya babu ya mtoto huyo kushauri waende kupimwa Hospsitali kupata
ukweli, ndipo baba huyo alipokubali kuwa anatembea na mtoto wake.
Kutokana
na kukubali kwake kwa mume wa mama huyo kwa kuhofia kwenda kugundulika
kutokana na vipimo kuonyesha ukweli hivyo alitakiwa kulipa adhabu ya
faini ya ng’ombe wawili,ambao aliwalipa na suala hilo kuwa limekwisha.
Hata hivyo pamoja na familia ya upande wa mama huyo kutokubaliana na maamuzi hayo ya kifamilia
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwina Bundala Makelema alikiri
kuwepo kwa suala hilo na kwamba wakati mtuhumiwa huyo akilipa adhabu
ya kimila ya ng’ombe wawili yeye alishiriki.
Leave a Comment