MZEE WA MIAKA 80 AISHI KWA KULA UDONGO WA NYUMBA ANAYOISHI JIJINI DAR ES SALAAM
Mzee
aitwaye Athuman Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa
nyumba anayoishi kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu.
Kikongwe
huyo alikutwahivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa
wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia
akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa.
Baada
ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John
Kanguya na majirani zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha
Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari
alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo.
Alisema
anawashukuru majirani wa eneo hilo ambao wameweza kutambua maisha
magumu anayoishi na kuamua kumpeleka hospitali na kumsaidia chakula.
alisema kikongwe huyo.
Leave a Comment