
Wachunguzi wa Kijerumani dhidi ya ndege ya
abiria ya Malaysia ambayo ilipata ajali huko Ukraine mwezi July na
kuripuka angani wanaeleza kua ndege hiyo baada ya kukumbwa na kitu
chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali ndio
chanzo cha ajali.
Mwandishi wa BBC amesema kwamba ushahidi huo ni
wawazi na kwamba ndege hiyo ilishambuliwa kwa kombora..katika ripoti yao
ya kwanza ya kiuchunguzi ,maafisi wa kijerumani katika masuala ya
usalama wa anga wameeleza kua hakukuwa na tatizo la kiufundi
lililosababisha ndege hiyo ipate ajali, ama makosa ya rubani
yalosababisha ndege aina ya MH17 kuripuka.
Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurikodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.
Abiria
wote miambili na tisini na nane walipoteza uhai pindi ilipo anza safari
kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala Lumpur.kutokana na
ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua
ndege hiyo.Lakini mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na
ajali hiyo.
Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 inaweza kupatikana pindi mwakani.
Leave a Comment