MKUU WA KITUO CHA POLISI (OCS) AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA AKIMBAKA MWANAFUNZI...!!!!
ALIYEKUWA Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyamboge katika wilaya na Mkoa
wa Geita E:2837 D/C Venance anashikiliwa na Polisi mkoani humo kwa
tuhuma za kukutwa akimbaka mwanafunzi.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio,
Mkuu huyo wa Kituo alimfanyia unyama huo mwanafunzi huyo
(18), anayesoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari Nyamboge.
Imeelezwa kuwa juzi mkuu huyo wa kituo alimtuma mmoja wa ‘vijana’
kwa ajili ya kuzungumza na mwanafunzi huyo, ili akubali kufanya mapenzi
naye mapenzi lakini mwaanafunzi huyo alikataa kwamba hawezi kwenda
nyumbani kwake (Askari).
“Mwanafunzi huyo alimweleza kijana aliyetumwa kwamba hawezi kwenda
nymbani kwa OCS,na kwamba kama anamhitaji amfuate chumbani kwake (Geto)
ili akapate hicho anachokihitaji….” shuhuda aliieleza
“Baada ya OCS kupata majibu hayo alikwenda hadi chumbani kwa
mwanafunzi huyo ambaye amepanga chumba kutokana na kuishi kijiji kingine
mbali na ilipo shule hiyo, lakini kumbe alikuwa amekwishawaeleza
wenzake juu ya namna anavyotendewa na OCS….” shuhuda wetu alizidi
kufafanua.
Inadaiwa kuwa OCS alifika chumbani hapo majira ya saa mbili usiku
na baada ya kuingia ndani mmoja wa vijana anayesoma na mwanafunzi huyo
ambaye alikuwa ameombwa na mwanafunzi wa kike kumsaidia alikwenda
kufunga mlango kisha kupiga yowe kuomba msaada.
“OCS aliposikia yowe aliamua kuvunja mlango lakini wakati anatoka
nje akakamatwa na wananchi ambao tayari walikuwa wameitikia yowe na
kuanza kumshambulia; hata hivyo polisi waliwahi kufika eneo la tukio na
kumuokoa…..” chanzo chetu kilieleza.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Joseph Konyo amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari jeshi hilo limefungua jalada la
uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa ingawa hatua ya kwanza waliyochukua ni
kumvua cheo alichokuwa nacho.
“Ni kweli hilo tukio lipo, tunaendelea kumshikilia hadi pale
tutakapojiridhisha na kila aina ya ushahidi tunaouhitaji; tayari
tumechukua hatua za awali ikiwa ni kumvua nyadhifa yake aliyokuwa nayo
na tumeshaanzisha mashitaka ya kijeshi dhidi yake…” Kamanda Konyo
alisema
“Taarifa tulizopokea ambazo hata yeye amekiri ni kwamba kweli
alikuwa akihitaji mahusiano na mwanafunzi huyo na mbinu aliyoitumia ni
baada ya kuamuru mwanafunzi huyo aachiwe kutokana na mashitaka
yaliyokuwa yakimkabili kituoni hapo….” Konyo aliongeza.
Akifafanua, Kamanda Konyo alisema askari wawili wa kituo hicho
walimtia mbaroni mwanafunzi huyo kwa tuhuma za kufanya mapenzi na
mwalimu wake na kwamba walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba
mwanafunzi huyo alikuwa anatembea na mwalimu wake.
Alisema baada ya suala hilo kufikishwa mbele ya OCS alimuita
mwanafunzi na kumwambia anamsaidia ili afutiwe shitaka lakini akaweka
sharti la kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo.
“Inavyoonekana mwanafunzi alikubali kwa sababu alikuwa kwenye
matatizo lakini alipotoka akaanza kumpiga chenga OCS na ndipo akaamua
kufanya uamuzi huo kwa sababu hakupendezeshwa; kuna madai kwamba
alipoingia alianza juhudi za kumbaka lakini wananchi waliwahi kufika
madai ambayo tumeanza kuyachunguza…” Aliongeza kamanda Konyo.
Kwa mujibu wa kamanda Konyo Askari huyo atashitakiwa kijeshi na
baada ya kesi yake kukamilika atafikishwa katika mahakama za kiraia.
Leave a Comment