KOCHA NOOIJ KUTAJA KIKOSI STARS

Na Boniface Wambura, Dar es salaam
 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij kesho (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.