HISTORIA YA SIKUKUU YA VALENTINE’S



Historia ya sikukuu ya Valentines na muanzilishi wake yaani mtakatifu valentine imejaa utata mwingi.Tunajua kwamba kwa miaka mingi mwezi wa pili umesherekewa kama mwezi wa mapenzi na hasa siku hii Valentine’s sikukuu hii ya valentine tunaweza sema asili yake ni mchanganyiko wa sikukuu ya kikristo na sikukuu itokanayo na mila za Kirumi (ancient roman empire) ni vyema tujue mtakatifu valentine ni nani na anahusiana vipi na mila za kirumi,au laa,basi pande hizi mbili zakutana vipi kuwa kitu kimoja.
Kanisa la Roman katoliki linawatambua watakatifu watatu walioitwa Valentine au Valentinus, Ambao wate waliteswa na kuuwawa kwa kukataa kuikana imani yao ya kikristo.Inasemekana kwamba Valentine alikua ni padri wa kanisa la Roman enzi zile za mwaka wa tatu za utawala wa kirumi.Wakati ambao mfalume Claudius wa pili aliona kwamba wanaume ambao hawajaowa ni wanajeshi bora kuliko wanaume walio owa ,hivyo alipitisha sheria iliyozuia wanaume kuowa. Lakini Valentine aliona sharia hiyo haikua na haki,akaamua kuvunja sharia ya mfalme na kuendelea kufungisha ndoa za vijana wapendanao kwa siri.Mfalme aliposikia habari zake aliamuru auwawe.
Inasemekana kwamba wakati Valentine amefungwa akisubiri hukumu ya kifo ndipo alipotuma salam zake za kwanza za ‘Valentine’baada ya kumpenda kimapenzi binti kipofu ambae alikua ni mototo wa Bwana jela,Binti huyo alimtembelea gerezani mara kwa mara wakati wa kifungo chake.Inasemekana kwamba kabla hajauwawa Valentine alimuandikia binti huyo barua na mwishoni aliandika”Kutoka kwa Valentine wako” kwa lugha ya kigeni “from your Valentine”Msemo ambao hata leo bado unatumika pale mtu anapotuma salamza valentine kwa maandishi..Ingawa bado kuna utata juu ya ukweli kuhusu muanzilishi wa sikukuu ya valentine,kila hadithi utakayo sikia juu yake inaonyesha alikua mtu mwenye Huruma,shujaa,na zaidi ya yote ni mtu aliependa kuonyesha mapenzi.Kutokana na sifa zake,kati ya karne ya tano na ya kumi na tano Valentine alikua moja kati wa watakatifu wenye jina kubwa sana nchini Wingereza na Ufaransa.
Asili ya siku ya Valentine’s: Sikukuu ya wapagani mwezi February
Wakati kuna watu wanaamini kua sikukuuya valentine inasherekewa katikati ya mwezi wa pili kama kumbukumbu ya kifo cha mtakatifu Valentino kilichotokea kwenye miaka ya A D 270-Wengine wanadai kwamba kanisa la kikristo liliweka sikukuu hiyo katikati ya mwezi wa pili katika juhudi zao za kuibadili sikukuu ya Lupercalia kua sikukuu ya kikristo.Lupercalia ilikua ni sikukuu ya wapagani iliyosherekewa na wafugaji kati ya tarehe 13 na 15 ya mwezi wa pili,ni matambiko yaliofanyika ili kuondoa roho wachafu katika mji na kukaribisha afya njema na uwezo mzuri wa kurutubisha,sherehe hizi ziliku rasmi kwa ajili ya mungu wa kilimo wa kirumi aliyeitwa Faunus.
Katika sikukuu hii,walichinja Mbuzi na Mbwa kama kafara,na damu ya mbuzi ilipakwa kila mtaa, ngozi ilichovywa katika damu kisha kila mwanamke na shamba lilipigwa kibao na ngozi hiyo yenye damu,wakiamini kua kufanya hivyo kutafanya mwanamke awe na uzazi mzuri na mashamba pia yatatoa mazao mazuri mwaka utakaofuatia.Na jioni baada ya matambiko hayo mabinti ambao hawajaolewa waliweka majina yao ndani ya kibuyu katikati ya mji na baadae kila kijana ambao hajaowa alichagua jina moja kutoka kwenye kibuyu ,jina ambalo alipata ndio mwanamke ambae alitakiwa kumuowa mwaka uliofuatia.Hapa ndipo dhana ya rangi nyekundu wakati wa sikukuu ya valentine ilipotokea

Sikukuu ya Valentine’s: Siku ya mapenzi
Mwishoni mwa karne ya tano,Sikukuu ya Lupercalia ilifutwa ki sharia kwani ilikua na maadili yasio ya kikristo.Papa Gelasius aliitangaza rasmi tarehe 14 ya mwezi wa pili kama sikukuu ya mtakatifu Valentine,yaani Valentines day.Miaka michache baadae sikukuu hiyo ilibeba maudhuhi au uzito wa mapenzi zaidi.Kati ya karne ya tano na karne ya kumi na tano,nchini wingereza na ufaransa ,iliaminika kwamba tarehe 14 ya mwezi wa pili ilikua ndio mwanzo wa kipindi cha ndege kupandana,hii ilijenga dhana kwamba siku ya sikukuu ya valentine lazima iwe siku ya kuonyesha mapenzi (romance).Ndio maana ndege hutumika kama alama ya Valentine.

Salama za valentine zilikua za kawaida sana enzi izo,lakini hapakua na salam za maandishi adi mwaka wa 1400 ambapo ndipo salama za kwanza za valentine ziliandikwa .Salam za valentine za zamani ambazo zipo adi leo ni shairi la Charles Duke wa Orleans,alillomuandikia mken wake mwaka 1415 akiwa gerezani huko London.Miaka michacha baadae,inaaminika kwamba Mfalme Henry wa Tano alimuajiri Muandishi John Lydgate amuandikie salam za Valentine kwa ajili ya Catherine Valois
imagesCAG6YZ4Q
Salam za valentine’s
Toka karne ya 15 ,salam za valentine’s zimekua zikibadilika kutoka kwenye uandishi wa mtu binafsi hadi kwenye ununuaji wa kadi maalum za salam hizo,pia sikukuu ya valentine imeambatanishwa na utoaji wa zawadi kwa wale wapendanao.Ingawa sikukuu hii ina uasilia wa mapenzi ya wapenzi,ni wazi kwamba tangu apo mwanzo sikukuu hii imekua ni kwa ajili ya watu wote wapendanao na si wapenzi tu.

Unaweza ukawa unajiuliza kwanini rangi nyekundu,ndege ,mauwa na chocolate ni vitu vinavyoibeba siku ya valentine’s.Hapo mwanzo nimekwisha kwambia juu ya rangi nyekundu na juu ya ndege.Tangu pale chocolate ilipogundulika ilihesabika kama kitu chenye thamani kubwa,yaani,(niseme kwa kiingereza ili upate maana kamili) Valuable,divine and decadent.Kwa sifa hizo ilionekana ni zawadi nzuri inayomstaili mwanamke. Mauwa Rose mekundu.kama yalivyo mauwa rose ya rangi nyingine linamaana yake.Uwa rose jekundu husema “NAKUPENDA” ikiwa na maana kwamba unampenda yule uliyemtumia,pia maua hayo ni ishara ya Romantic love and Enduring passion.

Naamini umeifuraia Article hii kama mimi nilivyofurai kukuandikia
Usiwasahau wazazi na ndugu zako katika sherehe izi za valentine.Nawatakia Valentine’s njema na yenye furaha.Nawapenda wote.
rose two
Happy Valentine’s
From your Valentine

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.