JINSI YA KUEPUKA UGONJWA WA KISUKARI
Kisukari Ni Nini?
Kisukari
ni ugonjwa unaotokana namtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye
damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe
kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Matokeo
ni kuharibiwa kwa viungo muhimu na hitilafu ya mzunguko wa damu, na
nyakati nyingine unaweza kufanya mtu akatwe vidole vya miguu au mguu,
pia husababisha upofu, na maradhi ya figo.
Wagonjwa wengi wa kisukari hufa kutokana na mshtuko wa moyo au kiharusi.
UGONJWA
wa kisukari unaongezeka haraka sana hivi kwamba umekuwa janga la
ulimwenguni pote. Kuna aina mbili kuu za kisukari. Aina ya kwanza huanza
hasa utotoni, na kufikia sasa madaktari hawajui jinsi ya kuizuia.
Makala
hii inazungumzia aina ya pili, ambayo imeathiri asilimia 90 ya watu
walio na kisukari. Ingawa zamani aina ya pili ya kisukari ilihusianishwa
tu na watu wazima, hivi karibuni imewaathiri pia watoto. Lakini
wataalamu wanasema kwamba mtu anaweza kujikinga ili asipatwe na
kisukari. Huenda ukafaidika kujua habari Fulani kuhusu ugonjwa huu
hatari.
Mafuta
mengi kupita kiasi mwilini huchangia sana kisukari. Wataalamu wanaamini
kwamba mafuta yaliyokusanyika tumboni na kiunoni ni ishara ya uwezekano
wa kupatwa na kisukari. Kihususani, mafuta katika kongosho na ini
huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.
Unawezaje kuepuka kupatwa na kisukari?
Hatua Tatu Zinazoweza Kukusaidia Usipatwe na Kisukari
1. Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu ikiwa una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari.
Mara nyingi aina ya pili ya kisukari huanza baada ya hatua inayoitwa prediabetes,yaani, ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu.
Hatua hiyo ni hatari kama tu kisukari, lakini kuna tofauti: Ingawa ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa,
hauwezi kutibiwa. Kwa upande mwingine, watu walio na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu wamefaulu
kukipunguza. Huenda mtu asitambue dalili za ongezeko la sukari kwenye damu. Kulingana na ripoti mbalimbali,
karibu
watu milioni 316 duniani pote wana kiwango kikubwa cha sukari kwenye
damu; ingawa wengi wao hawajui wana kiwango hicho. Kwa mfano, nchini
Marekani pekee asilimia 90 ya watu wenye sukari nyingi kwenye damu
hawatambui kama wana tatizo hilo.
Ingawa
hivyo, ongezeko la sukari kwenye damu ni hatari. Mbali na kuwa
kisababishi cha kisukari, hali hiyo imehusianishwa na hatari ya kupatwa
na ugonjwa wa akili uitwao dementia. Kama wewe ni mnene kupita kiasi,
hufanyi
mazoezi kwa ukawaida, au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda
tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Unaweza kujua kiwango
chako cha sukari ukipimwa damu.
2. Kula vyakula vyenye lishe.
Unaweza
kufaidika ukifanyamamboyafuatayo: Punguza kiasi cha chakula
unachokula.nBadala ya kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi au vinywaji
vyenye kaboni kama vile soda, kunywa maji, chai, au kahawa. Kula vyakula
vya nafaka ambayo haijakobolewa badala ya vyakula vilivyochujwa sana
viwandani. Kula nyama isiyo na mafuta mengi, samaki, njugu, karanga, na
maharagwe.
3. Fanya mazoezi.
Kufanya
mazoezi kunaweza kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu na kukusaidia
uwe na uzito unaofaa. Mtaalamu fulani anapendekeza kupunguza muda
unaotumia kutazama televisheni ili uwe na muda wa kufanya mazoezi.
Huwezi kubadili chembe zako za urithi, lakini unaweza kubadili maisha
yako. Utafaidika sana ikiwa utajitahidi kutunza afya yako
‘NILICHUKUA HATUA!’
Mahojiano
Ulijuaje kwamba ulikabili hatari ya kupatwa na kisukari?
Nilipofanyiwa
uchunguzi wa kitiba kabla ya kuanza kazi mpya, daktari aliniambia
ningepatwa na kisukari ikiwa nisingechukua hatua. Nilikuwa na mambo
manne yanayochangia kisukari:
Nilitoka
kwenye jamii ya watu wanaopatwa sana na kisukari, watu wangu wa
ukoowalikuwa na kisukari, nilikuwa mnene kupita kiasi, na sikufanya
mazoezi. Kwa kuwa singebadili mambo mawili ya kwanza, niliamua
kurekebisha mambo mawili ya mwisho.
Ulifanya nini?
Nilienda kumwona mtaalamu wa kisukari ambaye alinifafanulia uhusiano kati ya vyakula, mazoezi, uzito,
na
kisukari. Niliamua kubadili maisha yangu. Nikaanza kula mboga kabla ya
kula chakula kingine. Hilo lilinipunguzia njaa hivyo sikula sana. Pia,
nilianza kufanya mazoezi, jambo ambalo nilikuwa nimepuuza kwa miaka mingi.
Je, ulifaulu?
Kwa
kipindi cha miezi 18, nilipunguza asilimia kumi ya uzani wangu, na
ninahisi vizuri sana. Nimeazimia kwamba sitaishi tena kama zamani.
Hupaswi kucheza na kisukari!
Leave a Comment