Kero ya kukatika kwa umeme, Tanesco yawapoza wananchi
Shirika la umeme nchini Tanzania (Tanesco) limekanusha vikali suala la kuwepo mgao wa umeme katika sehemu mbali mbali jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mhandishi Mahenge Mugaya amesema kwamba tatizo la kukatika kukatika kwa umeme mara kwa mara kuanzia machi 15 ni uchakavu wa miundombinu ya umeme ikiwemo kuanguka kwa nguzo za umeme hususani katika maeneo ya makazi ya watu yasiyopimwa.
Ameongeza kuwa shirika la umeme nchni limetenga bajeti ya shilingi bilioni 10 katika mpango wa miaka mitatu wa kuimarisha umeme katika jiji la Dar es Salaam, mpango utakaowezesha kuondoa nguzo mbovu, miti iliyokatika njia za umeme na kuimarisha vituo vidogo vya kusambaza umeme.
Katika hatua nyingine amesema kuwa shirika hilo limeshafanya tathimini ya nguzo mbovu zote katika njia za umeme na kuandaa mpango kazi ili kuwa na mfumo mzuri wa usambazaji umeme
Leave a Comment