10 wafariki kwa ajali ya basi la Unique Shinyanga
Basi la kampuni ya Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso jana alasiri na lori la kampuni ya Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye mkoani Shinyanga.
Katika ajali hiyo watu 10 wamefariki na 50 wamejeruhiwa. Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wamesema kuwa dereva wa lori alikuwa anaendesha gari katikati ya barabara huku dereva wa basi akiwa katika mwendo kasi na katika kukwepa, basi hilo aligonga tela la lori kisha kupinduka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha kutokea tukio hilo lilihusisha watu 10 kupoteza maisha katika ajali hiyo kati yao 9 walifariki dunia papo hapo huku majeruhi 50 wakiwemo wanawake 13, wanaume 36 na mtoto mmoja wa kiume wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Leave a Comment