Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo.
1.Demu wako wa zamani
Ni vizuri
kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya
mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni
kwamba hakikamwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea
kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu
vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini
utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha
sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.
2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana na
kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza
kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila
pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa
hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa
mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale
ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo
patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.
3.Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli,
kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila
mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema
kuwa salamakuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja
kuyajutia kwa maisha yako yote.
4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa mbali nao,
labda kama unatakasalio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini
hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.
5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini
urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa
demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya
yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine
inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba
ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.Wadau mademu wapo
wengi sana, fanya kutafuta wengine nje ya hawa.
Leave a Comment