KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KIKAO CHA BAJETI YA SHIRIKA LA MAGEREZA KWA MWAKA 2015/2016 LEO MKOANI MOROGORO
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(suti nyeusi) akisalimiana na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja mara baada ya
kuwasili leo Mei 25, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema, Mkoani
Morogoro kwa ajili ya ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la
Magereza kwa Mwaka 2015/2016(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak
Abdulwakil(hayupo pichani) kutoa hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Bajeti
ya Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016.
Wajumbe wa Kikao cha Bajeti ya
Shirika la Magereza kwa Mwaka 2015/2016 wakifuatilia kwa makini hotuba
ya mgeni rasmi leo Mei 25, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema,
Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja akimkabidhi Begi lenye makabrasha ya Kikao
cha Bajeti ya Shirika la Magereza, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma
za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Wajumbe wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka
2015/2016 waliosimama(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na
Utawala, Gaston Sanga(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Leave a Comment