Aina 12 za wanaume ambao binti hata awe mjanja vipi atakutana nao katika maisha yake
Faida zake
- Hukufurahisha na ya kukusisimua
- Hufanya ucheke
- Anakua pembeni yako kwa kila jambo na atakupigania na kukulinda
Hasara
- Mara nyingi wanatabia za kunywa pombe na kuvuta sana sigara
- Kila mra hakosi drama za kukushangaza
- Atakuwa katika hali hiyo ya ukorofi milele
- Kushikwa na kuwekwa jela ni kawaida yao kutokana na drama zao
- MR. KWA SASA SINA MSICHANA
Faida zake
- Atakuchukua na kukutoa out kila mara
- Atakutambulisha kwa marafiki zake wote
- Atakuwa ni mtu wa kukupa pongezi wakati wote
Hasara
- Anamchumba ambaye wako naye kwa muda mrefu
- Hawezi kukuambia kuwa ana mchumba
- Baada ya kuteka moyo wako nawe umedata ndio atakuambia kuwa ana mpenzi
- MR. MAARUFU
Faida zake
- Atakupa fedha nyingi na hakuna kukulizwa maswali
- Ana style nyingi za jinsi anavyoendesha maisha yake
- Atakuonyesha baadhi ya mambo mazuri katika maisha yako
Hasara
- Kamwe usije jaribu kuishika simu yake
- Anamaamuzi ya kutokukushirikisha, anaweza kuja nyumbani kwako wakati wowote bila kutoa taarifa
- Anapenda kuwa karibu na marafiki zake zaidi kuliko wewe.
- MR. MISHEMISHE A.K.A JEMBE
Faida zake
- Anaweza kukupa mialiko wewe na marafikio zako katika minuso mbalimbali na kumbi nyingi za
- Unaweza kuwa na heshima na kila uongeacho na kuchochea mazungumzo pia
- Anavaaa nguo za gharama
Hasara
- Huwezi kujua kama yeye ni shoga au lah kwani hana kazi, muda wote yupo kwake na huoni dalili za kuhangaika lakini ana maisha mema na pombe kila siku
- Hujifanya anakuwa mkali ukijaribu kumwelezea juu ya mpango wa mahusiano yenu kwenda mbele
- Ukiwa bado kwenye mstari wa kupata tiketi uingie kwenye pati, au mnuso unaweza kushuhudia drama pale mlangoni na kisha mkaruhusiwa kuingia
- Ana rundo la picha za yeye na celebrities kibao lakini hawajuani na mmpoja kati ya hao mastaa
- MR. MSOMI
Faida zake
- Muda wote yupo smart
- Anakujali na kuhakikisha unajisikia vyema
c.Ana kazi nzuri sana
hasara
- Mambo yake yanaboa sana kwani muda mwingi anahangaika na mambo ya kazi
- Hata kwa bed ni mvivu sana kwana anakuwas kachoka na majukumu
- Hayuko smart sana na mambo ya mtaani kama kukutoa out kwani anakuwa busy
- Daima ni mtu wa kukuliza lini tutaonana tena
- MR. GETO
Faida zake
- Hukufanya ucheke
- Anavutia kuwa naye karibu
- Ana hasira za haraka, lakini kwa ujumla ni mtu poa
- Atasema yeye anataka uhusiano wa kweli
Hasara
- Ana watoto 3 au zaidi kwa mama tofauti
- Anataka kukutumia apate chakula, fedha za matumizi na sio upendo
- Na kila ukimwambia ukweli juu ya mambo yake anakataa au kuwa mkali
- Kama ukikaa naer anaweza rudi hata saa tisa usiku na kujitetea alikuwa na marafiki
- MR. RASTA
Faida zake
- Atakufundisha mambo mengi ya upendo na amani
- Yeye ni mwanaharakati au mwanamapinduzi
- Atakupa maneno na falsafa zenye kukupa msukumo wa amani na ni maneno ya kihalisa yenye hisia
- Anataka mke na familia
Hasara
- Atakupiga chini akipata binti wa kizungu
- Ana hela za kufanyia starehe ila hana kazi maalumu
- Haimiliki suti nzuri, siku zote amevaa kombati au jinsi na kutokwa na jasho
- Mwishoni utagundua kuwa alikuwa anakuigizia
- MR. FUTURE
Faida zake
- Atakutambulisha kwa mama yake
- Ana kazi na atakuwa mtu wa kujirusha na wewe
- Atakupa fedha za mahitaji yako kama unahitaji
- Wakati mwingine huenda kanisani Jumapili
Hasara
- Wakati mwingine naye anataka kuwa mtu wa kuishi free
- Ni mtu wa kuvaa mikufu na saa fake
- Kuna wakati yeye yuko busy na kufuatilia michezo aipendayo na kukusahau wewe kama upo
- Baada ya kuachana ndio utagundua alikuwa ana mabinti kibao.
- MR. KICHECHE
Faida zake
- Atakuambia ukweli – kwamba wewe sio mmoja tu kwake
- Yeye atakwambia kwamba umembadilisha na yuko tayari kutulia na wewe
- Anakaa kwake ana usafiri na atakuomba uhamie pale make wote
Hasara
- Hawezi kukutambulisha kuwa wewe ni mpenzi wake mkiwa sehemu hasa akiona kuna wanawake
- Kwa ujumla yeye ni mzushi wa kila afanyacho
- Anatarajia wewe kuamini uongo wake wote kwa sababu tu alikuambia ukweli kuhusu wanawake wengine alipkuwa nao
- Baada ya kumdaka uongo wake atajitetea alishakuambia kuwa alikuwa kicheche
- MR.NINA KAZI NZURI
Faida zake
- Bila shaka ana kazi
- Hana tabia nyingi mbaya sana
c.Atachukua wajibu wa kukuhudumia wewe wakati wewe ni mgonjwa
- Atakwambia kwamba yeye ana upendo wa dhati na wewe
Hasara
- Utadumu naye katika uhusiano wa miaka 2 au zaidi na kisha unakuja kugundua ni mvivu, mpuuzi na bedui ambaye anataka wewe kufanya kazi zote za mke lakini si kukupa pete.
- Atamaliza kwa kukuambia anakupenda ila wewe sio chaguo lake
- Baada ya kukuacha miezi mitatu baadae anafunga ndoa
- MR. RAFIKI WA UHAKIKA
Faida zake
- Yeye ni rafiki yako bora, uamweleza kila kitu kinachokusibu na mnakwenda pamoja vizuri sana
- Anatoa ushauri kwa wakati unapopatwa na matatizo
- Ni mwanaume wa kweli
- mwelewa na anakujali na ni mcheshi wa kupindukia
Hasara
- Manishia kujirusha na mwishowe unakuja kugundua hana lolote yeye anataka sex basi.
- Hapo unahitaji kupata mpenzi mpya kwani yeye hana mpango wa maisha na wewe
- MR. MWANAUME SAHIHI
Faida zake
- Yeye anampenda Mungu na anachukua uhusiano wake na Mungu kwa umakini
- Yeye ni mwelewa, ana kipaji na uwezo wa kukuchukua wewe kiakili na kihisia
- Naye atakupenda hata wakati wewe haupendeki
- Yeye ana ujuzi wa kufanya kazi kwa ustadi na anapendwa !
- Anakubali makosa yake na inajitahidi kuwa mtu bora
- Anaelewa uhusiano unajengwa kwa 200% . Yeye100% na wewe 100%
- Yeye hana kundi la watoto wa mama, yeye ni nadhifu zaidi na anakitambua.
- Yeye ni rafiki wa bora wa kweli na kila kitu unachotaka kwa mwanaume yeye anacho
- Alikuwa mzuri ulivyokutana naye ila baada ya kukaa naye unagundua anazidi kuwa nadhifi zaidi
- Anaweza kupangilia mavazi – anajua tofauti kati ya mavazi rasmi , ya kawaida, ya kitaaluma, ya biashara
- Yeye anampenda mama yake na kuheshimu wanawake
Hasara
- Hujawahi kutana naye na kama yupo basi ana mke au mchumba .
- Yeye hataki uhusiano wowote kwa sasa
- Umeshamsikia sana mtu wa aina hii lakini kamwe hujakutana naye na lazaidi umeshakutana na aina hizo hapo juu za wanaume na wakakuchezea vilivyo
Leave a Comment