Aina za mahusiano

Moja kati ya vitu vya kuvutia wakati ukikuwa ni kuingia kwenye uhusiano uliopevuka. Mkichezacheza na ukitumia muda na mtu wa kipekee kwako huwa inafurahisha; Hatahivyo kadri unavyozidi kuwa mkubwa unaweza kuona uhusiano huo unachanganya kidogo. Kuna uhusiano wa aina nyingi. Kujifunza kuhusu mapenzi na kuvutiwa na mtu, ni furaha kwa wakati unakuwa, lakini ni muhimu kujua kuna mahusiano mengine yenye athari ambazo unatakiwa kuziepuka.

Kuvutiwa: Wakati mwingine ni ngumu sana kujua kama unampenda mtu kweli. Mapigo ya moyo yanaongezeka unajiona unakosa pumzi na unasikia kizunguzungu ukimuona mtu fulani. Unaanza kudhani hayo ni mapenzi. Unashindwa kujizuia. Lakini baada ya muda mawazo hayo yanapotea. Hii inaitwa kuvutiwa na mtu. Kuvutiwa na mtu ni kitu cha kawaida kabisa.

Mapenzi: Ni ngumu kueleza mapenzi ni nini, yanajumuisha hisia mbalimbali. Kwa ujumla Mapenzi ni hisia za ndani za kuvutiwa, kupendezwa, kumheshimu, kumjali na kumuelewa mtu mwingine, licha ya mapungufu yake. Mapenzi ya kweli yanajumuisha hisia za kuwajibika na kujitoa kwa ajili ya mtu mwingine. Pale unapokuwa unampenda mtu kwa dhati basi mnaheshimiana.

Urafiki: Siku hizi ni kawaida kwa wasichana na wavulana kuwa marafiki: hata hivyo urafiki huo huwa unachanganya kidogo pale mnapokuwa wakubwa. Ili kuendelea kuwa na urafiki wa karibu sana mnatakiwa kuwasiliana vizuri ili kuhakikisha wote mnaelewana sana. Kuna wakati mwingine mnatakiwa kuepuka presha ya makundi ili kuepuka urafiki wenu kuwa tofauti na hali ya halisi.

Fataki: Hakuna tatizo kwa wanawake kuwavutia wanaume kupokea zawadi kutoka kwao, lakini unatakiwa kujua nyuma ya zawadi hizo anataka nini. Wakati mwingine wanaume wanaweza kudai malipo ya zawadi alizokupa na akaanza kukushawishi mfanye ngono. Hii siyo sahihi! Mara zote unauamuzi wa kuamua ufanye au usifanye ngono na mtu. Unatakiwa kuthamini utu wako na kujithamini dhidi ya vitu vya kupita tu. Mafataki wanapenda kuwinda wasichanaau wavulana wadogo ambao wanaamini kuwa hawawezi kusema hapana. Wanakosea. Unahaki ya kuchagua na unasauti ya kusema hapana kwa Mafataki.

Inachanganya!: Kuwa kwenye uhusiano na mtu ambaye yuko kwenye uhusiano na watu wengi ni hatari kwa afya yako na usalama wako. Uhusiano wenye nguvu ni ule kati ya watu ambao wako wazi wanapokuwa pamoja na wanaolindana.

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.