HAYA NDIYO MAAJABU YA MWANAMKE

Imagine……
ANAKUFUMANIA:
Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza, anakuelewa,
anakusamehe – halafu anasahau.
UNAZAA NJE YA NDOA:
Anasononeka na kulia
sana. Anachukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa
upendo. Kama ni kuchukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI:
Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi
chakulaalichokuandalia bila manung’uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER:
Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU:
Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna
maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!
UNAJIANDAAA KWENDA KIBARUANI:
Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama ya askari trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwausafi! Ulichomuudhi jana
kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO:
Anauthamini, anautunza
anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina,Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!
Na mengine meeeenggggiiiii i sana wanafanyiwa hawa watu lakini
WANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani!
HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

No comments

Theme images by sbayram. Powered by Blogger.