TANZANIA HATARINI KUKUMBWA NA MAFURIKO YA EL-NINO
Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja
wa Mataifa umetahadharisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi kadhaa
ambazo zinauwezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko yatakayosababishwa
na El- Nino.
Kwa
mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na
Misaada ya Ki-binadamu na Uratibu wa Misaada ya Dharura, Bw Stephen
O’Brien, kipindi ambacho Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya
El-Nino ni kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu wa 2016.
Nchi nyingine ambazo zinauwezekano wa kukumbwa na mafuriko makubwa pamoja na Tanzania ni Madagascar, Malawi na Msumbiji.
Taarifa
ya Bw. O’Brien kuhusu madhara ya El-Nino na namna gani Jumuiya ya
Kimataifa inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na kadhia hiyo
iliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa
Mataifa na nakala yake kutumwa kwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, pamoja na kutoa tahadhri hiyo, amewasihi nchi
ambazo zinatarajiwa kukubwa na maafa ya El -Nino kujiandaa
ipasavyo.
Maandalizi hayo ni pamoja utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wananchi watarajiwa wa athari za El- Nino .
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi, kwa upande wa Afrika ya
Mashariki, nchi kadhaa hususan ukanda kwa magharibi zimekubwa na
uhaba mkubwa wa mvua na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa
chakula. Nchi hizo ni Ethiopia Sudan, Djibouti na Eritrea, ili hali
baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka mipaka.
“
Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania, Msumbiji,
Madagascar na Malawi zinauwezekano mkubwa kwa kukubwa na mafuriko ya
El- Nino” . anatahadharisha O’Brien
Kwa mujibu wa Bw. Stephen O’Brien hichi hizo zitahitaji pamoja na
mambo mengine misaada ya kujiandaa na kushughulikia ya kile
kinachotabiliwa kwamba kinauwezekano mkubwa wa kutokea.
Ukiacha
nchi za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine kwa upande wa Afrika ambazo
zinakumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua na hivyo kutishia usalama na
upatikanaji wa chakula ni Angola, Botswana, Malawi, Namibia, Afrika
ya Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
Nchi
hizi zimekubwa na uhaba mkubwa wa mvua kiasi kwamba na kwa mujibu mwa
Bw. Stephen O’Brien zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ambapo watu
zaidi ya milioni 28 katika mataifa hivyo watakabiliwa na uhaba wa
chakula
Akizungumzia
kuhusu misaada ambayo imekwisha kutolewa na nchi wahisani katika
kukabiliana na ukame na madhara yatokanayo na El-Nino , Katibu Mkuu
Msaidizi Mwandamizi anasema kuwa hadi wakati anatoa taarifa yake kiasi
cha dola 360 milioni kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la
kukabiliana na madhara yatakayotokana na El-Nino ukiwamo usalama wa
chakula.
Pamoja
na michango hiyo, Bw. O’Brien anasema haitoshi kutokana na ukweli
kwamba maafa yatakayotokana na madhira ya El-Nino yanahitaji misaada
zaidi
Mbali
ya nchi za kanda ya Afrika baadhi ya nchi ulimwenguni ambazo
zinatakumbwa na ama zimeshakubwa na balaa la El-Nino ni pamoja na Nchi
ambao zimo katika Bara la Latini ya Amerika, na nchi za eneo
la Pacific ambazo nyingi ni visiwa.
Shirika
la Kimataifa la Hali ya Hewa ( World Meteorogical Organization)
litanatarajiwa katika mwezi February kutoa taarifa zaidi kuhusu
mwelekeo wa El-Nino
Leave a Comment