KAMA WEWE NI MWANANDOA JITAHIDI UYAJIBU MASWALI HAYA
2. Mmeoana na mwenzako kwa muda gani?
3. Kabla ya kuoana, mlifahamiana au kuwa marafiki kwa muda gani
4 Je unaridhika jinsi mwenzako (mkeo/mumeo) anavyohusiana/ishi na ndugu zako?
5. Kama jibu la swali namba nne hapo juu ni (b) au (c), kwa nini huridhiki?
6. Kuna wakati mmewahi kutofautiana/kugombana na mwenzako sababu ya ndugu?
7. Kama jibu la swali namba sita ni ndio, ni kwa kiwango gani swala la mahusiano ya mwenzako na ndugu zake/zako linakusumbua?
8. Kama jibu la swali namba sita ni ndiyo, unafikiri au ungependa mwenzako afanye nini ili kuepusha ugomvi wakati mwingine? Eleza hapa
9. Kama kuna migongano/ugomvi katika ndoa yenu, unafikiri mahusiano na ndugu yana mchango mkubwa kiasi gani?
10. Je mna mgawanyo wowote wa majukumu nyumbani?
11. Kama jibu la swali namba 10 ni ‘ndiyo’, mgawanyo huo mlikubaliana au ilitokea tu?
12. Unaridhika na mwenzako anavyotekeleza majukumu yake ya nyumbani (Mfano: watoto, mahitaji, usafi, chakula, nk)?
13. Kama jibu la swali namba 12 ni ‘Hapana’, je ungependa mwanzako akufanyie/afanye nini?
14. Kama kuna migongano/ugomvi katika ndoa yenu, unafikiri majukumu ya nyumbani yana mchango mkubwa kiasi gani?
15. Je unaridhika na tendo la ndoa katika mahusiano yako na mwenzako?
16. Kama jibu la swali namba 15 hapo ni (c) au (d), unafiriki kwanini huridhiki?
17. Tendo la ndoa ni muhimu kiasi gani kwako?
18. Je mmeshawahi kutofautiana/kugombana na mwenzi wako sababu ya tendo la ndoa?
19. Kama ni migongano/ugomvi katika ndoa yenu, unafikiri tendo la ndoa lina mchango mkubwa kiasi gani?
20. Kama ungependa mabadiliko katika tendo la ndoa ungependa mwenzako afanye nini? Elezea
21. Je unamwamini mwenzi wako kwa asilimia mia moja?
22. Kama jibu la swali namba 21 ni ‘hapana’, ni kwanini humwamini, au kwanini unashaka naye? Tafadhali elezea
23. Je umewahi kutoka nje ya ndoa yako? (uwe huru na wazi kusema ukweli, kumbuka hujataja jina mahali popote)
24. Kama jibu la swali namba 23 ni ‘ndiyo’, je umetoka nje ya ndoa mara ngapi?
25. Kama jibu la swali namba 23 ni ‘ndiyo’, unadhani ni sababu zipi zilikufanya ukatoka nje ya ndoa?
26. Kama jibu la swali namba 23 hapo juu ni ‘hapana’, je umewahi kushawishika/kuwaza kuwa siku moja unaweza kutoka nje ya ndoa?
27. Kama jibu la swali namba 26 hapo juu ni ‘ndiyo’, sababu gani zimekufanya uwaze kuwa siku moja unaweza kutoka nje ya ndoa? Eleza
28. Kama umewahi kutoka nje ya ndoa, na hutamani iendelee kuwa hivyo, unafikiri mweza wako afanye nini ili usiendelee kutoka nje ya ndoa tena? Elezea
29. Kama kuna migongano na magomvi katika ndoa yenu, unafikiri uaminifu katika ndoa una mchango mkubwa kiasi gani?
30. Je mahusiano baina ya mwenza wako na marafiki zake au wafanyakazi wenzake yamewahi kusababisha ugomvi au kutokuelewana kati yenu?
31. Kama jibu la swali namba 30 ni ‘ndiyo’, Eleza ni kwajinsi gani mahusiano hayo yalisababisha kutokuelewana kwenu?
32. Kuna maoni yeyote ungependa kutoa kuhusu mahusiano ya mwenza wako na marafiki zake au wafanyakazi wenzake? Kama ndiyo, tafadhali elezea hapa.
33. Je unamweka mwenza wako katika kiwango kipi kuhusiana na suala la uwazi wa kipato chake katika mahusiano yenu?
34. Je unaridhika na jinsi mwenza wako anavyotumia fedha/kipato anachopata? Kama jibu ni hapana, kwanini huridhiki? Elezea
35. Je mmewahi kutofautiana/kugombana na mwenzi wako sababu ya matumizi mabaya ya fedha? Kama ndiyo, tafadhali elezea
36. Kuhusiana na swala la fedha na mali, tafadhali jibu kwa kuweka vema katika kifungu kimojawapo hapa chini.
37. Kama jibu la swali namba 36 ni ‘a’, au ‘b’, unafikiri kwanini mwenza wako anakunyanyasa? Elezea
38. Kama kuna migongano au magomvi katika ndoa yenu, unafikiri suala la fedha na mali linachangia kwa kiasi gani?
39. Kama una maoni yeyote ambayo ungetaka kumwambia mwenza wako kuhusu swala la uwazi katika fedha na mali zenu ungemshauri nini?
40. Je unafikiri mna mawasiliano yaliyo bora na yakutosha baina yenu ninyi wawili?
41. Je unaweza kuyaweka mahusiano yenu katika ubora upi kati ya maelezo haya hapa chini?
42. Je mmewahi kugombana au kutofautiana kwa sababu ya suala zima la mawasiliano
43. Kama jibu la swali namba 42 ni ‘ndiyo’, suala la mawasiliano lilisababisha vipi kutofautiana huko? (Elezea)
45. Kama kuna migongano/ugomvi katika ndoa yenu, unafikiri suala la mawasiliano linachangia kwa kiasi gani?
46. Kama kuna maoni au ushauri wowote ambayo ungetaka kumwambia mwenza wako kuhusu hali ya mawasiliano baina yenu ungemwambia nini?.
47. Je kuna tabia binafsi yeyote ambayo mwenzi wako anayo tofauti na ambazo zimezungumziwa hapo juu ambayo imekuwa chanzo cha kutokuelewana kwenu? Tafadhali ieleze/zieleze hapa
48. Unafikiri mchango wa tabia hiyo/hizo binafsi katika kugombana au kutofautiana kwenu ni kwa kiasi gani?
49. Umewahi kufanya jitihada zozote katika kurekebishana kwenye hizo tabia? Elezea
50. Je unafikiri kwa tatizo lolote lililoelezwa hapo juu, umechangia kwa namna yeyote kwa mwenzako kuwa na tatizo hilo?
51. Je unafikiri unafanya juhudi kubwa kiasi gani katika kuboresha ndoa yenu?
52. Kama umefanya juhudi kubwa katika kuboresha ndoa yenu, juhudi zako zimefanikiwa kwa kiwango gani?
53. Waweza kuelezeaje mahusiano yako na mwenzako kabla ya ndoa hasa kipindi cha uchumba?
54. Je mliwahi kufanya tendo la ndoa kabla ya kuingia katika ndoa?
55. Kama jibu lako hapo juu (swali no. 54) ni ndiyo, Je?...
56. Unadhani kuna changamoto zozote mnazozikabili kwenye ndoa yenu kwa sasa ambazo chanzo chake ni mahusiano yenu kabla ya ndoa? Elezea
57. Iwapo mlifanya tendo la ndoa kabla ya ndoa, unadhani limeleta athari gani kwenye maisha yenu ya ndoa. Elezea
58. Unamwonaje mwenzako kuhusiana na mambo haya hapa chini
59. Je mtizamo wako kuhusu ndoa yenu ni upi kati ya mitizamo hii?
60. Je ungepewa nafasi na uhuru wa kuachana na mwenzako ungefanya hivyo?
61. Je umewekeza namna gani katika ndoa yako (kwa jinsi moyo wako ulivyozama kwenye penzi lenu)
62. Je ungepewa nafasi ya kuchagua tena mume/mke, ungemchagua tena huyo uliye nae sasa?
63. Je ungepewa nafasi ya kutoa talaka ungempa mwenzako talaka?
64. Unafikiri suluhisho la matatizo/tofauti katika ndoa yenu ni nini? Elezea unavyo fikiri
65. Unafikiri mwenzako anajali na kushiriki malezi ya watoto wenu kiasi cha kutosha? Elezea
66. Kama kuna chochote ambacho ungependa kumshauri mtu mwingine aliyeko kwenye ndoa kama wewe ungemwambiaje? Elezea.
67. Ungepewa nafasi ya kumshauri mtu ambaye anampango wakuingia katika mahusiano ya ndoa hivi karibuni ungemwambiaje?
Asante sana
Leave a Comment