MAMBO 5 YANAYORUDISHA NYUMA BIASHARA YAKO
Kama ilivyo ada, wafanyabiashara wengi;
wakubwa kwa wadogo, nchini Tanzania na kungineko duniani hupenda husimamia
kukuza soko(ongezeko la wateja) na kujiongezea faida. Si jambo la kubeza hata kidogo
kuwa ongezeko la faida litokanalo na ongezeko la wateja ni msingi wa kukuza
biashara yako.
Takwimu
zinaonyesha kuwa kati ya biashara mpya 100 zilizoanzishwa ni 5 pekee
hudumu kwa miaka 5 na nyingine hufa katika kipindi cha miezi 6 ya
utendaji, nyingine kati ya miaka 2 na nyingine miaka 3.
Wakati huu, yamezekana nimekuandikia makala hii wewe uliye na Kampuni/Biashara yenye umri zaidi
ya miaka 3 na bado ipo vile vile ….yaani wewe ni kutembeza nguo miaka nenda
rudi (Mfano wa mfanyabiashara mdogo).Vipi
siku nguvu zikiisha za kutembea kwa miguu?, ikiwa ni hivyo kuna tatizo na
unapaswa kujiuliza kwanini biashara yako haikui.
Mara nyingi napenda kusisitiza kupitia msemo
maarufu wa Kiuchumi kutoka kwa Jim Rohn kuwa “People get paid for bringing value
to the marketplace”…yaani kwa tafsiri ya Lugha ya Kiswahili; Watu hulipwa
kutokana na uthamani wauletao kwenye soko.Soko linalozungumzwa hapa ni “watu”;
ni kukidhi maumivu ya wateja/ uhitaji wa wateja.
Katika harakati za kukuza wigo wa biashara,
iwe kubwa au ndogo, kuna mambo ya msingi sana ya kuzingatia. Haitoshi kuendelea
kuzalisha/ kuuza bidhaa au kutoa huduma bila kuzingatia uhitaji wa wateja kwa
wakati husika, hivyo kila wakati ni vyema kujua kuwa inampasa mfanyabiashara
kujifunza kufanya/kuendesha biashara yake katika mfumo usio wa kawaida wa
kimazoea…ni lazima kufanya biashara nje ya mfumo ili kukidhi uhitaji wa soko
kwa wakati husika.Ubunifu unahitajika sana! hasa katika mfumo huu wa soko huria wenye ukuaji wa kasi wa teknolojia.
Kupitia ufafanuzi huo, yafuatayo ni mambo (5)
nyeti ambayo kwa hakika yanarudisha na pia yamerudisha nyuma ukuaji wa biashara
nyingi.
1.KUENDESHA
BIASHARA KIMAZOEA- Kuamini zaidi katika njia fulani pekee katika kuendesha
biashara na kusahau kuwa mahitaji ya wateja yanaweza kubadilika kutokana
uhalisia wa maisha kwa wakati husika.
2.KUKOSA
UBUNIFU
(Kuiga na si kuboresha mapungufu ya wengine)...hivi sasa nchini
Tanzania, kila mtu anafikiria kuwa Wakala wa Makampuni makubwa mfano:
Simu, Bima na Benki. Simaanishi kuwa ni vibaya, lakini ni vyema
kujiongezea ubunifu binafsi.
3.KUDHARAU
WATEJA
WAPYA (Kuridhika na wateja waliopo kwa kuwa faida inaonekana kwa
waliopo).Huku ni Kujisahau au nasema ni kulala fofofo! Ili kuzinduka
usingizini, ulizia makampuni haya makubwa yaliyowahi kuwepo duniani-
“Kodak” na “Sony”, yapo wapo? na yanafanya nini kwa sasa? ukilinganisha
na uhitaji wa soko na kukua kwa teknolojia.
4. KURIDHIKA
NA AINA KADHAA ZA
BIDHAA/HUDUMA( kuamini kuwa bidhaa/huduma fulani ndiyo iliyolishika
soko, hivyo hatubanduki hapo.Ni vyema kukidhi matakwa kwa wateja kwa
wingi kulingana na uhitaji wao.
5.KUDHARAU
KUJIHAKIKI,
HAKUNA MALENGO YA MUDA MREFU-“Ignoring reinvention”.Tambua kuwa kila
baada ya mwaka unaitathmini na kuhakiki biashara yako, kinyume na hapo
mambo yanabadilika kwa kasi na unaiweka biashara hatarini.Pia weka
malengo ya muda mrefu ya biashara yako yakisaidiwa na malengo ya muda
mfupi.
Leave a Comment