Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa
katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri
juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika
shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama
mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka
penzi la mwanamke.
KUBEMBELEZWA
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao
hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na
misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe
nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa
zaidi kuliko kufokewa.
KUWA NAMBA MOJA
Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha
kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni
zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa
namba moja au kupendwa.
Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa
kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla. Wanawake
hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa
na wanawake wenzao wabaya.
KURIDHISHWA KWENYE TENDO
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako
kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi
lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake
katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.
MAZUNGUMZO
Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume
wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa
wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa msingi
huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza
mawazo yao. Kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na kumsikiliza
bila kumkatiza kwa ukali.
Leave a Comment