DALILI ZA KUJUA KAMA UKO NA MWENZI SAHIHI

Kila siku ni valentine, huo ndio mwendelezo wa kukua vizuri kwa mahusiano yalio imara bila ya kujali vyeo .kutafuta hekima na maarifa katika safari hii ya ya kujifunza jinsi ya kujipenda na kupenda wengine .
kuna watu wengi wanauliza kuwa nitajuaje kama nipo na mke sahihi?
kwanza inabidi kufahamu kwanza, na kujiuliza kwa nini nahitaji mahusiano. na je yatafika wapi!,
watu wengi hufanya kupata wenza kwa sababu
1.kupata mapenzi , ulinzi,uthibitisho , usalama na kupata mtoto , au mtu wa kukamilisha na kujaza upweke alionao ili ajisikie mkamilifu na kuwa mwenye kustahili kwa sifa.
2.hutaka kuwa na mapenzi na mtu, au kupata kampani ili azidi kukuza hisia zake za kimwili.
Inabidi kwanza wewe uwe ni mtu ulie sahihi ndio utakapopata mtu sahihi , huwezi kupata mtu sahihi ikiwa wewe sio sahihi, au unaweza kupata mtu sahihi lakini wewe ukawa sio sahihi. ina maana kwamba lazima kwanza wewe uwe ni mwenye kujipenda ndipo utapenda na wengine
Pia ujifunze kuwa mtu mkamilifu ili uje kupata mtu alie mkamilifu. kwa hio inabidi uwe na maswali mengi kabla hujaanza kuchukua maamuzi ya kutafuta mtu sahihi.Jiulize , umekamilika au ni tamaa tu inakupeleka kutafuta mtu wa kukukampani.?
kama nia yako ni kupata mapenzi tu , basi hapo bado hujakamilika, lazima uwe na kazi kubwa ya kufanya ndani ya moyo wako kabla .unahitaji kupata kazi ya kujifunza kujipenda , na kujifunza majukumu ya kupenda wengine, uwe na hisia za kujisikia mkamilifu na usalama za namba moja, yaani kupata na kutoa.
jiulize maswali yafuatayo.
1.je mtu ulie nae ni muwazi kiasi cha wewe kujifunza kitu kwake?
mtu muwazi ni rahisi kjifunza kujua kama anajipenda na kuwapenda wengine, lakini mtu wa kificho ni vigumu kujua , na hutaweza kujifunza kitu kwake. uwazi ni chombo cha msingi sana katika mahusiano yeyote. hata kama kuna migogoro ni rahisi kurekebisha baina yenu . lakini watu wenye kificho ni ngumu hata kama kuna migogoro wanakuwa na hasira , hufoka , huhamaki, wanakuwa na hisia kali za kimwili zaidi. kwa hio sio sahihi.
2.ni mtu anyethubutu kujali na ni mwenye huruma na uelewa na mtu wa kukubalika na anakubali jinsi ulivyo. kukosekana kwa uelewa ni dalili ya moja kwa moja kuwa sio sahihi
3.unapata zile hisia za msingi , zile cheche zinazokuvuta kwake? unapenda kuwa karibu nae? unapenda jinsi alivyo?
Inawezekana ana harufu fulani hupendi, kama huna hizi hisia ndani ya miezi 6 ya kuwa na huyo mtu basi hakufai, uelewe huyo ni rafiki tu wa kupita hawezi kuwa mwenza wa maisha .
4. je anajitahidi kulazimisha ili awe sahihi?
unaweza kuwa ,mnafanya vitu kwa pamoja , lakini bado unaona kama kuna upungufu fulani kwako huyomsio mtu sahihi kwako, hata ukijitahidi vipi huwezi kufika mbali nae.
5.mnashirikiana katika kipato chenu?
mnakubaliana katika matumizi?, uzazi, kula manunuzi ya vitu, mazoezi,usafi na kuwajibika kwa pamoja na mnaelewana?.
6.Mna imani moja ? na labda wote mnapenda siasa?
hiki ni kinyume cha kujifunza kuwa sahihi na kuwa wazi , hapo unatakiwa umakini sana, kuna watu huwa wanaficha tabia zao kwa kuwa wanataka kuolewa au kuoa.
7.je huyu mtu ameathirika na kitu chochote?katika maisha yake ambacho ametumia labda kimemharibu. kama vile madawa ya kulevya , labda aliwahi kubakwa , kunyanyaswa, ,labda mlevi wa pombe, au anapenda tv, au instagram, internet n.k
ukimpenda mtu lazima upende na kila kitu alichonacho, jinsi alivyo, lakini ujue kuwa wote tumeumizwa na kitu fulani katika maisha na kila mmoja anhita kupata nafuu kwa mwenzake usitegemee mabadiliko ya mtu , umepata ulichoona. lakini ukiwa na subira unaweza kuwa na matumaini ya kubadilika. lakini pia kumbuka sio sahihi.
Inabidi ukubaliane na hilo au uamue kuondoka, kwanini? kwa sababu kutegemea kubadilika unweza kupata magonjwa ya moyo.
kumbuka: unatakiwa kwanza wewe uwe mwenza sahihi ndipo utakapopata mwenza sahihi. tunavutwa na hisia za kawaida za mahitaji ya muda na kujipenda mwenyewe, ni bora ujipende kwanza .
bora ubadilike na kujua zaidi upendo wa kweli katika mahusiano ili uwe kamili katika maisha yako yote.
toa mawazo yako katika hili hili kusaidia wengine
Leave a Comment